Taasisi ya McKinsey Global imetoa ripoti ikisema kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka 2017, utegemezi wa dunia kwa uchumi wa China uliongezeka kutoka 0.4 hadi 1.2. Haya ni matokeo yanayotarajiwa ya maendeleo ya utandawazi duniani, na yameonyesha kuwa katika mchakato wa kujiunga na dunia, China imehimiza ukuaji wa uchumi wa dunia, na imani ya jumui ya kimataifa kwa uchumi wa China inaongezeka.
Kwa mujibu wa hesabu za Benki ya Dunia, kuanzia mwaka 2012 hadi mwaka 2016, mchango uliotolewa na China kwa ongezeko la uchumi wa dunia umefikia asilimia 34, kiasi ambacho kimezidi mchango wa jumla uliotolewa na Marekani, Ulaya na Japan kwa pamoja. Hii ndiyo sababu ya kuongezeka kwa utegemezi wa dunia kwa uchumi wa China.
Kwanza, China ina soko kubwa zaidi na idadi kubwa zaidi ya watu wenye kipato cha kati duniani, na watu hao wanahitaji sana bidhaa za ngazi ya juu, mambo hayo yametoa injini kwa ukuaji wa uchumi wa dunia. Mashirika mbalimbali yamekadiria kuwa mwaka 2030, ongezeko la manunuzi ya bidhaa nchini China litafikia dola za kimarekani trilioni 6, kiasi ambacho ni cha jumla katika Marekani na nchi za Ulaya Magharibi.
Pili, China ni nchi pekee duniani yenye aina zote za viwanda, na mlolongo wa utoaji bidhaa nchini una nguvu bora ya kipekee. Kwa upande mmoja, mlolongo wa utoaji bidhaa wa China umepunguza gharama kwa kampuni za kimataifa na zile zinazoagiza bidhaa kutoka China, na kuzivutia ziwekeze nchini China; kwa upande mwingine, bidhaa za China zinazouzwa nje ya nchi zinajumuisha raslimali na vipuri vingi vinavyoagizwa kutoka nchi nyingine, na hii inasaidia kukuza uchumi wa nchi hizo.
Tatu, uwekezaji wa China nje ya nchi umetoa mchango muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa dunia. Mwaka jana, China iliwekeza dola za kimarekani bilioni 120 nje ya nchi, kutoa nafasi za ajira milioni 17 katika nchi nyingine, na kusaidia kuongeza kodi ya dola za kimarekani bilioni 40. Uwekezaji wa China umetoa manufaa halisi kwa nchi hizo, na hii bila shaka inasaidia kuimarisha uhusiano wa kiuchumi kati ya China na nchi hizo.
Hivi sasa, sera za kujilinda na upande mmoja zinaendelea kutandika, na kutishia muundo wa viwanda wa dunia na utulivu wa mambo ya fedha, na sintofahamu zinazoukabili uchumi wa dunia zinaongezeka kidhahiri. Katika mazingira hayo, China inaimarisha mageuzi na kufungua mlango wake ili kuendelea kuwa "chombo cha kutuliza" uchumi wa dunia.
Historia ya miaka 40 tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango imeonyesha kuwa, bila ya dunia, China haiwezi kupata maendeleo, na dunia pia inaihitaji China kupata ustawi na utulivu. Ndio katika mchakato wa kujiunga na dunia, China inazidi kuonesha umuhimu wake katika kuongeza manunuzi ya bidhaa, kutoa bidhaa na mitaji. Katika siku za baadaye, China itaendelea kufanya vizuri mambo yake, na kutoa mchango mpya kwa ajili ya ukuaji wa uchumi wa dunia.