Viongozi wapya wa Umoja wa Ulaya watarajiwa kuhimiza uhusiano kati ya Umoja huo na China
2019-07-09 18:07:58| CRI

Rais Xi Jinping wa China leo amemtumia salama za pongezi waziri mkuu wa Ubelgiji Bw. Charles Michel kwa kuteuliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Baraza la Ulaya. Katika barua hiyo, rais xi amesema China inaunga mkono Ulaya kufanya kazi muhimu zaidi katika mambo ya kimataifa, na kupenda kuhimiza uhusiano wa kiwenzi kati ya pande hizo mbili katika masuala ya amani, maendeleo, mageuzi na ustaarabu.

Mkutano maalumu wa wakuu wa Umoja wa Ulaya uliofanyika wiki iliyopita uliteua viongozi wanne wa Umoja huo. Waziri mkuu wa Ubelgiji Bw. Michel atakuwa mwenyekiti wa baraza la Ulaya, waziri wa ulinzi wa Ujerumani Bi. Ursula von der Leyen atakuwa mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Ulaya, mwenyekiti wa Shirika la Fedha Duniani Bi. Christine Lagarde kutoka Ufarasa atakuwa mkuu wa Benki Kuu ya Ulaya, na waziri wa mambo ya nje wa Hispania Bw. Josep Borrell Fontelles atakuwa mwakilishi mwandamizi wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia sera za diplomasia na usalama.

Hivi sasa Umoja wa Ulaya unakabiliwa na changamoto mbalimbali, zikiwemo suala la wakimbizi, nguvu ya kisasa inayojali fikra kali za umma, kukwama kwa Brexit, kudidimia kwa uchumi, na mvutano wa kibiashara na Marekani, hivyo kuimarisha na kuongeza ushirikiano na China ni mwekeleo wa juhudi za kidiplomasia ya Umoja wa Ulaya.

Mwaka huu, rais Xi Jinping na waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang kwa nyakati tofauti walifanya ziara barani Ulaya. Kwenye mkutano wa 21 wa wakuu wa China na Umoja wa Ulaya uliofanyika Aprili, pande hizo mbili zilisisitiza kusukuma mbele zaidi uhusiano wa kiwenzi kati yao katika mambo ya amani, maendeleo, mageuzi na ustaarabu, na kupanga kwa pamoja ajenda ya ushirikiano baada ya mwaka 2020.

China na Umoja wa Ulaya zina lengo la pamoja katika kulinda amani duniani. Kutokana na ongezeko la vitendo vya kujilinda kibiashara na upande mmoja, China na Umoja wa Ulaya zinatetea kulinda utaratibu wa kimataifa ambao kiini chake ni Umoja wa Mataifa, kuunga mkono kutatua migogoro ya kikanda kwa njia ya mazungumzo, na kuhimiza kwa pamoja amani, utulivu na maendeleo endelevu duniani.

Katika masuala ya ongezeko la uchumi na mageuzi, China na Umoja wa Ulaya pia zina maslahi mengi ya pamoja. Umoja wa Ulaya umekuwa mwenzi mkubwa zaidi wa kibiashara wa China kwa miaka 15 mfululizo, ambapo China pia ni mwenzi mkubwa wa pili wa kibiashara wa Umoja huo. Kutokana na mvutano wa kibiashara unaochochelewa na Marekani, pande hizo mbili zinapaswa kushirikiana ili kulinda utaratibu wa pande nyingi na biashara huria.

Katika mazungumzo ya ustaarabu, ushirikiano kati ya China na Umoja wa Ulaya pia unaongezeka. Mwezi Machi mwaka huu, rais Xi alipofanya ziara barani Ulaya, alifikia makubaliano mengi na viongozi wa Italia, Ufaransa, na Monaco katika mambo ya utamaduni, michezo, elimu, utalii na sekta nyinginezo.

Hivi sasa dunia inakabiliwa na mabadiliko makubwa, na maslahi ya pamoja ya China na Umoja wa Ulaya zinaongezeka kwa mfululizo. China inapenda kushirikiana na viongozi wapya wa umoja huo kuinua zaidi kiwango cha uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya pande hizo mbili katika miaka mitano ijayo.