Uchumi wa China waendelea kwa utulivu
2019-07-15 20:49:44| CRI

Takwimu mpya zinazotolewa na idara ya takwimu ya taifa ya China zimeonesha kuwa, katika nusu ya kwanza ya mwaka huu pato la taifa la China limezidi dola trilioni 6.5 za kimarekani, ambalo ni ongezeko la asilimia 6.3 ikilinganishwa na mwaka jana. Katika hali ambayo uchumi wa dunia unakabiliwa na hatua yz upande mmoja na kujilinda kibiashara, uchumi wa China umeendelea kwa utulivu na ukuaji wa uchumi huo una sifa ya juu zaidi.

Tangu mwaka jana kutokana na ongezeko la mambo yasiyo na uhakika na utulivu, shinikizo la kupungua linaloukabili uchumi wa China liliongezeka. Kiwango cha asilimia 6.3 cha ongezeko la uchumi wa China kipo katika eneo la lengo la asilimia 6 hadi 6.5 lililowekwa na serikali ya China ambacho kinalingana na matarajio ya mabadiliko ya mitindo ya maendeleo ya uchumi wa China, kutoka ukuaji wa kasi hadi ukuaji wenye sifa ya juu.

Ingawa hivi sasa nchi nyingi bado hazijatangaza takwimu za uchumi za nusu ya kwanza ya mwaka, lakini kutokana na makadirio husika ya mashirika ya kimataifa kiwango cha asilimia 6.3 cha kasi ya ongezeko la uchumi wa China kinaweza kuongoza katika makundi makuu ya kiuchumi duniani. Hivi sasa, mchango wa China katika uchumi wa dunia umefikia asilimia 30, katika siku za baadaye China itaendelea kuwa injini kuu ya kuhimiza ongezeko la uchumi wa China.