China kuzidi kulinda hakimiliki za ujuzi katika pande nyingi
2019-07-18 20:38:34| CRI

Idara ya hakimiliki za ujuzi ya taifa ya China hivi karibuni imetangaza hakimiliki mpya ya ujuzi ya kampuni ya Huawei, ambayo ni "njia na vifaa vya kielektroniki vya kupiga picha za mwezi". Baada ya hapo, mkutano wa kawaida wa baraza la serikali ya China uliofanyika jana, umeamua kuchukua mfululizo wa hatua ili kuzidi kuimarisha nguvu ya kulinda hakimiliki za ujuzi. Uvumbuzi wa China unaendelea kwa kasi, na ulinzi wa hakimiliki za ujuzi ukiwa nguvu kubwa zaidi ya kuhimiza uvumbuzi pia unapiga hatua kubwa. Kutokana na hatua mpya, China itazidi kuimarisha ulinzi wa hakimiliki za ujuzi katika pande nne:

Ya kwanza ni kudumisha kuimarisha utekelezaji wa sheria wa hakimiliki za ujuzi na kuchukulia kwa usawa maslahi halali ya mashirika na wadau mbalimbali wa soko. Hii inamaanisha kuwa katika mchakato wa utekelezaji wa sheria, China inatumia vigezo vya pamoja na mchakato wa pamoja kwa mashirika na wadau wote katika soko. Wakati huohuo, China pia itahimiza kutoa nyaraka za sera kuhusu ulinzi wa hakimiliki za ujuzi, na kusukuma mbele kazi ya kuzidisha nguvu ya kupambana na vitendo vya ukiukaji wa hakimiliki.

Ya pili, China itahimiza marekebisho ya sheria ya hakimiliki, sheria ya hakimiliki za ujuzi na sheria ya alama za biashara, na kuinua kwa kiasi kikubwa adhabu dhidi ya vitendo vya ukiukaji wa sheria.

Ya tatu, ili kuungana na vigezo vya kimataifa, China itaendelea kuinua sifa na ufanisi wa ukaguzi wa hakimiliki za ujuzi, huku ikiweka bayana kuwa itapunguza kipindi cha kukagua hakimiliki zenye thamani ya juu hadi miezi 17.5 na muda wa ukaguzi wa wastani wa usajili wa alama za biashara ndani ya miezi mitano.

Mbali na hayo, China itazidi kuimarisha ushirikiano wa kimataifa kuhusu ulinzi wa hakimiliki za ujuzi, ili kuyarahisishia mashirika kupata haki halali na kulinda haki zao.

Hivi sasa, binadamu wanakabiliana na fursa ya duru mpya ya mapinduzi ya sayansi na teknolojia na mabadiliko ya viwanda. Kulinda hakimiliki za ujuzi ni kulinda uvumbuzi. China itachochea nguvu ya uvumbuzi kwa kulinda hakimiliki za ujuzi, ili kutoa nguvu kwa maendeleo ya sifa ya juu katika mchakato wa kuzidi kuimarisha mageuzi na kupanua ufunguaji wa mlango.