Bunge la Ulaya jana lilipitisha azimio linalohusiana na Hong Kong, likiitaka serikali ya Hong Kong kuondoa mashtaka dhidi ya waandamanaji waliofanya vurugu bila ya sababu na kuanzisha uchunguzi kuhusu vitendo vya utekelezaji wa sheria vya polisi wa Hong Kong. Azimio hilo limepuuza vitendo vibaya vya kimabavu vilivyotokea hivi karibuni Hong Kong, na limekosa msimamo wa msingi wa utawala wa sheria na pia ni uchokozi mbaya kwa utaratibu wa utawala wa sheria wa Hong Kong na kuingilia siasa za ndani za China. China inalaani vikali na kupinga kithabiti azimio hilo.
Utawala wa kisheria ni msingi wa jamii ya Hong Kong. Hivi karibuni baadhi ya watu wenye msimamo mkali wa Hong Kong walishambulia jengo la baraza la sheria, kuziba njia na kuwashambulia askari polisi. Mabavu hayo ni vitendo vilivyopangwa na kuandaliwa, ambavyo vimevuka mpaka wa kueleza madai ya amani na kuvuruga vibaya utaratibu wa utawala wa kisheria wa Hong Kong. Nchi yoyote yenye mamlaka haiwezi kuvumilia hali hiyo. Wakati polisi wa Hong Kong wakitekeleza sheria, walikuwa wanajizuia kwa kiasi kikubwa ili kulinda utaratibu wa jamii, lakini walishambuliwa na waandamanaji hao. Hivi sasa askari 13 wa polisi wamejeruhiwa na wawili kati yao wamevunjiwa vidole.
Vitendo hivi vya kimabavu vimekosolewa na kulaaniwa jumuiya ya kimataifa. Lakini baadhi ya watu wa Ulaya wamechagua kupuuza mabavu hayo, na kuyaelezea kuwa maandamano ya amani, na sio tu wanaitaka serikali ya Hong Kong kuwafutia mashtaka wahalifu hao, bali pia wanachafua jina la polisi wa Hong Kong kwa kufanya utekelezaji wa sheria wa kimabavu. Vigezo viwili vinavyotumiwa kwa mabavu hayo, vimekiuka kanuni za msingi za uhusiano wa kimataifa, pia vimefichua uwongo wa Ulaya.
Hivi sasa, awamu mpya ya bunge la Ulaya imechaguliwa, uhusiano kati ya China na Ulaya unakabiliwa na fursa mpya ya maendeleo. Azimio hilo kuhusu Hong Kong lililopitishwa na bunge hilo si sheria, lakini limetoa ishara yenye makosa kwa nje na litaharibu maendeleo ya uhusiano kati ya pande mbili. Mambo ya Hong Kong ni siasa ya ndani ya China, nchi, shirika na mtu yoyote hana haki ya kuingilia. Uhusiano mzuri kati ya China na Ulaya unafuata maslahi ya pande mbili, Ulaya inatakiwa kushughulikia vizuri mambo yake, na kufanya juhudi pamoja na China kulinda maendeleo mazuri ya uhusiano huo.