Wanasiasa wenye hila wa Marekani hawana haki ya kulaani mambo ya kidini nchini China
2019-07-20 18:07:36| CRI

Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Michael Pompeo kwa nyakati tofauti wametoa hotuba ya kuipaka matope China katika mambo ya kidini.

Kwenye hotuba zao, Pence na Pompeo wamepotosha ukweli wa mambo, na kusema vituo vya mafunzo ya ajira kwa watu wenye msimamo mkali mkoani Xinjiang, China, ni kama jela ya kusafisha mawazo, na serikali ya China inakandamiza watawa wa budha mkoani Tibet.

Lakini ukweli ni kwamba, mkoani Xinjiang, kila waislamu 530 wana msikiti mmoja, na idadi ya misikiti mkoani humo imezidi elfu 24.4. Ili kuwasaidia watu wenye msimamo mkali kutokana na athari ya ugaidi, serikali ya Xinjiang ilianzisha vituo vya mafunzo ya ajira. Katika miaka mitatu iliyopita, hakuna matukio ya kigaidi yaliyotokea mkoani humo, na hali hii inaonesha kuwa vituo hivyo vimefanya kazi nzuri katika kukinga ugaidi. Mkoani Tibet, kuna zaidi ya mahekalu 1,700, na watawa elfu 46. Wakazi wa mkoa huo wana uhuru wa kutosha wa kuabudu.

Katika miaka ya hivi karibuni, wanadiplomasia wengi wa nchi za nje waliotembelea mikoa hiyo miwili wanaona kuwa, serikali ya China imefanya kazi zenye ufanisi katika kulinda haki za bindamu haswa kwa watu wa makabila madogo madogo. Hivi karibuni wajumbe wa kudumu wa nchi 37 katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva wameandika barua ya pamoja kwa mwenyekiti wa kamati ya haki za binadamu ya umoja huo, na kuipongeza China kwa kupata mafanikio makubwa katika kuendeleza haki za bindamu na kupambana na ugaidi mkoani Xinjiang.

Kwa upande wa Marekani, hadi sasa idadi ya misikiti kote nchini humo haijafikia asilimia 10 ya misikiti mkoani Xinjiang, China. Takwimu zilizotolewa na Shirika la Gallup zinaonesha kuwa, asilimia 42 ya wananchi wa Marekani wana wasiwasi kuhusu uhusiano wa kidini nchini humo, na asilimia 75 ya waislamu wa Marekani wanaona wanadharauliwa vibaya.

Wakiwa maofisa wa ngazi ya juu wa Marekani, Pence na Pompeo wangejishughulisha zaidi na mambo ya nchi yao, badala ya kuingilia mambo ya ndani ya China.