Soko la hisa la China lafungua ukurasa mpya
2019-07-22 19:12:30| CRI

Soko la hisa la China limefungua ukurasa mpya, baada ya hisa za kwanza za makampuni 25 ya teknolojia na uvumbuzi kuanza kuuzwa kwenye soko hilo leo asubuhi.

Mwezi Novemba mwaka 2018 rais Xi Jinping wa China kwenye maonesho ya kwanza ya bidhaa za nje zinazonunuliwa na China, alitangaza kuzindua sekta ya hisa za makampuni za teknolojia na uvumbuzi kwenye soko la hisa nchini China, ili kuhimiza mageuzi ya soko la mitaji.

Tofauti na sekta nyingine, katika siku tano za kwanza, mabadiliko ya bei ya hisa za makampuni ya sekta hiyo hayana ukomo.

Ikiwa hatua muhimu ya China katika kukuza mageuzi na kufungua mlango, kuzinduliwa kwa sekta hiyo kumeonesha nia, imani na hatua halisi ya China kuhusu mambo ya mitaji.