Vitendo vya umwamba vya Marekani vyaharibu utaratibu wa kimataifa
2019-07-24 16:40:38| CRI

Hivi karibuni zaidi ya wamarekani 100 wenye uhasama na China wamesaini barua ya pamoja ya kushutumu China kupuuza kanuni na utaratibu wa kimataifa, na kuchochea serikali ya nchi hiyo kupingana na China. Barua hiyo inapotosha ukweli, na kuonesha kuwa watu hao hawana uelewa mzuri wa mambo ya China.

Ukweli umethibitisha kuwa, vitendo vya umwamba vya Marekani vya upande mmoja, kujilinda kibiashara, kujilinda kimaslahi kupita kiasi vinaharibu utaratibu wa kimataifa.

Utaratibu wa kimataifa wa hivi sasa ulijengwa baada ya vita kuu ya pili ya dunia, na kwa jumla umefanya kazi nzuri, haswa mfumo wa usalama wa kimataifa ambao kiini chake ni Umoja wa Mataifa, umelinda vizuri amani na maendeleo ya dunia. Lakini Marekani siku zote inajichukulia kama kiini cha utaratibu wa kimataifa, ili kulinda maslahi yake yenyewe. Wakati inaposhindwa kutimiza malengo yake kupitia Umoja wa Mataifa, inajaribu kuharibu utaratibu wa kimataifa. Tangu awamu hii ya serikali ya Marekani kuingia madarakani, nchi hiyo imefanya hivyo mara nyingi.

Kwanza, Marekani imeinua fimbo ya ushuru, na kuanzisha mvutano wa kibiashara na nchi nyingi ikiwemo China, Mexico, Canada, nchi za Umoja wa Ulaya, na India, na kuleta athari kubwa kwa mnyororo wa uzalishaji duniani na utaratibu wa kibiashara ya kimataifa.

Pili, hadi sasa Marekani imejitenga kutoka kwenye Kamati ya Haki za Binadamu, Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, makubaliano ya Paris kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, na makubaliano kuhusu suala la nyuklia ya Iran, na pia imezuia kazi za Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki na mageuzi ya Shirika la Biashara Duniani. Licha ya hayo, Marekani pia inajaribu kujitoa kutoka kwenye sheria yoyote ya kimataifa.

Kwa upande mwingine, ikiwa moja ya waanzilishi, wanufaika na walinzi wa utaratibu wa kimataifa wa hivi sasa, China haina sababu ya kuharibu utaratibu huo. China imetoa mawazo ya kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja, na pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", wakati huohuo inalinda mamlaka ya Umoja wa Mataifa na kushiriki kwenye operesheni za kulinda amani kwa hatua madhubuti. Lengo la China ni kuhimiza nchi mbalimbali duniani zinapata mafanikio na maendeleo kwa pamoja.

Baadhi ya wanasiasa wa Marekani wanaharibu utaratibu wa kimataifa, na kukataa kutekeleza majukumu yao ya kimataifa, huku wakishutumu China kupuuza utaratibu wa kimataifa. Sababu yao kuu ya kufanya hivyo ni kwamba, utaratibu wa kimataifa unaolindwa na China si utaratibu wanaoupenda , hivyo wanataka kupaka matope China.

Hivi sasa dunia inakabiliwa na mabadiliko makubwa ambayo hayajatokea katika miaka 100 iliyopita, utaratibu wa kimataifa unapaswa kujadiliwa na nchi mbalimbali duniani badala ya nchi moja. Umwamba wa Marekani umepitwa na wakati, na utakuwa tishio na changamoto kubwa dhidi ya utaratibu wa kimataifa. Nchi zote zinapaswa kuwa na tahadhari, na kulinda utaratibu wa kimataifa kwa hatua halisi, na kuuhimiza uwe na haki na usawa zaidi.