Nchi ipi yakandamiza na kutishia nchi nyingine duniani?
2019-07-25 17:07:19| CRI

Hivi karibuni zaidi ya wamarekani 100 wenye uhasama na China wameandika barua ya pamoja kwa rais Donald Trump wa nchi yao, wakishutumu China kwa "kukandamiza na kutishia nchi nyingine kwa kutumia nguvu yake kubwa". Kauli hiyo imeshangaza watu wengi, ambao wanaona kuwa Marekani ni nchi inayokandamiza na kutishia zaidi nchi nyingine.

Kwenye barua hiyo, wamarekani hao wamesema, kinyume na China, katika mfumo wa taifa la Marekani, siasa ni mambo ya kawaida, na vita ni ya nadra. Lakini takwimu zilizotolewa na watafiti zinaonesha kuwa, katika miaka zaidi ya 200 iliyopita tangu kuanzishwa kwa Marekani, nchi hiyo imetumia asilimia 90 ya kipindi hicho katika vita. Hata katika mwaka wa mwisho wa muhula wa Barack Obama anayejulikana kama "rais wa amani", nchi hiyo ilitupa mabomu karibu elfu 26 katika nchi 7. Kwa upande mwingine, katika miaka 70 iliyopita tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, China haijaanzisha vita hata mara moja dhidi ya nchi nyingine.

Katika miaka ya hivi karibuni, kwa kisingizio cha ugaidi, Marekani ilianzisha vita dhidi ya Afghanistan, Iran na Syria, na kusababisha vifo na majeruhi ya raia wengi wa nchi hizo, pamoja na msukosuko wa wakimbizi. Tangu awamu hii ya serikali ya Marekani kuingia madarakani, imetekeleza sera za upande mmoja bila ya kujali maslahi ya nchi nyingine. Kwa mfano ilitambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel na kukiuka azimio la Umoja wa Mataifa na maoni ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa, ilijitoa kutoka kwenye makubaliano ya kimataifa kuhusu suala la nyuklia la Iran, na kuleta hali ya wasiwasi katika Mashariki ya Kati, na pia ilijitoa kwenye makubaliano na Russia kuhusu makombora ya masafa ya kati.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Taasisi ya kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Dunia ya Stockholm, mwaka jana, matumizi ya Marekani katika mambo ya kijeshi yalifikia dola bilioni 640 za kimarekani, na kushika nafasi ya kwanza duniani. Wakati huohuo, wastani wa matumizi ya kijeshi ya China kwa mtu ni sawa na asilimia 5 ya Marekani.

Hivi karibuni rais wa zamani wa Markekani Jimmy Carter alisema, Marekani ni nchi inayopenda zaidi vita duniani, na China haikutumia hata senti moja ya fedha zake katika vita. Naye waziri mkuu wa Malasiya Bw. Mahathir Mohamad amesema, nchi yake imedumisha uhusiano na China kwa miaka karibu 2000, na China haijawahi kujaribu kuvamia Malasiya bila kujali kuwa ina nguvu kubwa namna gani, kwani China haipendi kuumiza nchi nyingine. Ikiwa nchi inayopenda amani toka zama za kale, China ni mjenzi na mlinzi wa amani ya dunia. Hadi sasa China imepeleka askari zaidi ya elfu 37 wa kulinda amani katika sehemu zinazokumbwa na vita duniani, na licha ya hayo, China inabeba asilimia 15.22 ya bajeti ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya operesheni za kulinda amani.

Hivi sasa dunia inakabiliwa na changamoto mbalimbali. Zikiwa wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, China na Marekani zinapaswa kushirikiana vizuri katika mambo ya kimataifa, haswa masuala ya nyuklia ya Korea ya Kaskazini na Iran, na mgogoro wa Mashariki ya Kati. Ni wakati sasa wa Marekani kuacha kabisa mawazo ya vita baridi.