Uchambuzi: Marekani inakwamisha ushirikiano na maendeleo ya dunia
2019-07-26 19:30:28| CRI

Zaidi ya wamarekani mia moja wenye msimamo mkali dhidi ya China, hivi karibuni walimwandikia barua ya pamoja rais Donald Trump wa nchi yao, wakishutumu China kwa kuwashawishi washirika wa Marekani na nchi nyingine kwa mbinu za kiuchumi, ili kupanua ushawishi wake duniani. Ni wazi kuwa kauli hii inakashfu utetezi wa China wa kufanya maendeleo ya uchumi wake kunufaisha dunia nzima, na pia imeonyesha hisia za wivu na chuki ya baadhi ya wamarekani, na ongezeko la nguvu ya kiuchumi ya China. Lakini hali halisi ni kuwa sera ya upande mmoja na ya kujilinda wanayotetea wanasiasa wa Marekani, ndio kizuidi dhidi ya maendeleo ya pamoja kupitia ushirikiano kati ya nchi mbalimbali duniani.

Katika miaka ya hivi karibuni, Marekani imekuwa inatumia fimbo ya ushuru na kuweka vizuizi vya kibiashara hapa na pale, kuvuruga minyororo ya viwanda na thamani duniani na kusababisha hasara kubwa kwa biashara, uwekezaji na hata uchumi wa dunia.

Kuanzia tarehe 10, Oktoba mwaka jana, Marekani imepanua wigo wa uchunguzi kuhusu hatari ya uwekezaji wa kigeni katika sekta 27 kwa kisingizio cha "usalama wa taifa", na kuzilazimisha kampuni zitoe taarifa juu ya biashara zao, hatua ambazo zimepunguza imani ya wawekezaji wa kimataifa. Ripoti iliyotolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa imepunguza makadirio ya kasi ya ukuaji wa uchumi wa dunia kwa mwaka huu na mwaka kesho kwa asilimia 0.1 kuliko yale ya mwezi Aprili.

Wakati huohuo, sera ya umwamba wa kiteknolojia inayofuatwa na Marekani pia imezuia maendeleo ya teknolojia na ustaarabu ya binadamu. Kwa mfano, ili kugombania nafasi ya uongozi katika teknolojia ya hali ya juu kama vile mtandao wa 5G, Marekani imetumia nyenzo za kiserikali kukandamizi kampuni ya China na kuziagiza kampuni nyingi za Marekani zisitoe malighafi na teknolojia kwa kampuni ya China. Baadhi ya watu wanataka kutengana kwa teknolojia za China na Marekani, na hata kuzuia nchi nyingine kutumia teknolojia ya 5G ya China kwa njia mbalimbali na kwa kutoa ubembe wa maslahi mbalimbali.

Aliyekuwa naibu balozi wa Marekani nchini China na mkalimani mkuu wa rais Richard Nixon Bw. Charles Freeman, hivi karibuni alitoa makala akisema maendeleo ya teknolojia yanazitaka nchi mbalimbali kuimarisha ushirikiano, na Marekani itaharibu uwezo wake wa uvumbuzi kama ikizuia maendeleo ya teknolojia ya China, na juhudi za Marekani za kuiangusha China zinaweza kudhoofisha uchumi wa Marekani, wala sio kuzuia maendeleo ya China.

China ikiwa nchi inayowajibika, maendeleo yake sio tu yanakidhi mahitaji yanayoongezeka ya wananchi wake na maisha bora, bali pia yatazinufaisha nchi nyingine na wananchi wao.

Kwa miaka mingi mfululizo, China imeongoza duniani kwa kuchangia asilimia zaidi ya 30 ya ukuaji wa uchumi wa dunia. China inataka kuwa mchangiaji wa maendeleo ya dunia, hii inatokana na utamaduni wake wa "kufanya dunia nzima inufaike na mafanikio yako". Lakini ni vigumu kwa wanasiasa hawa wanaotetea "Marekani Kwanza" kuielewa.

Kama tujuavyo, mwaka 2013 China ilitoa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kwa lengo la kushikilia kanuni za kushauriana, kujenga kwa pamoja na kunufaishana, kuhamasisha rasilimali nyingi kuongeza mawasiliano, kupanua masoko, kuchimba nguvu za ukuaji wa uchumi na kuzifanya nchi na sehemu nyingi zijiunge na mafungamano ya kiuchumi.

Hivi sasa, maendeleo bado ni njia muhimu ya kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili binadamu. Marekani ikiwa nchi inayoongoza kiuchumi duniani inatakiwa kufanya juhudi za kupunguza pengo la maendeleo badala ya kuzuia maendeleo ya nchi nyingine. Mafungamano ya kiuchumi ni mwelekeo mkuu, na uwazi na ushirikiano ni mkondo wa karne hii, ambavyo haviwezi kuzuiliwa na baadhi ya wamarekani wanaoshikilia sera ya upande mmoja na ya kujilinda.