Ikulu ya Marekani Ijumaa ilimwagiza mjumbe wake wa mambo ya biashara achukue kila hatua awezayo ili kuhakikisha Shirika la biashara duniani WTO linafanya mageuzi juu ya hadhi ya nchi na sehemu wanachama zinazoendelea kwenye shirika hilo. Pia imetishia kuwa kama hakuna maendeleo yoyote yanayopatikana ndani ya siku 90, Marekani itachukua hatua yake ya upande mmoja. Kitendo hicho kinaonesha umwamba wa Marekani na jinsi inavyoidharau kanuni ya WTO.
Ifahamike kuwa kuainisha hadhi ya nchi na sehemu wanachama zinazoendelea kwenye shirika la WTO ni hatua iliyokuwepo kwa muda mrefu kwenye shirika hilo, ambayo inazipatia nchi na sehemu wanachama fursa ya kuhimiza mageuzi ya ndani na kufungua soko, pia inaweza kuhakikisha ongezeko endelevu la kiuchumi kwa wanachama hao. Lakini Marekani haipendi kanuni hiyo ya kimsingi ya WTO, inaona kuwa kanuni hiyo inazifanya nchi na sehemu zinazokua kwa kasi kiuchumi ziharibu maslahi ya Marekani.
Ukweli ni kwamba nchi na sehemu kuthibitishwa kuwa na uchumi unaoendelea hakutokani na kigezo kimoja tu, bali kuna vigezo vingi ikiwa ni pamoja na kiwango cha jumla cha uchumi, pato la taifa GDP, muundo wa sekta mbalimbali, uwezo wa uvumbuzi, mgawanyiko wa mapato ya raia n.k. China ni nchi yenye watu bilioni takriban 1.4, ambapo kiwango cha vigezo hivyo kwa kila mtu kimekuwa kidogo zaidi kuliko Marekani. Kitu cha msingi kwenye pengo kati ya China na Marekani kimekuwa pengo kati ya nchi kubwa zaidi inayoendelea na nchi kubwa zaidi iliyoendelea duniani. Marekani inachukua kiwango cha jumla cha uchumi wa China kiwe kigezo pekee cha kubatilisha hadhi ya nchi inayoendelea ya China, kitendo ambacho hakitakuwa na msingi wowote.
Kanuni ya utaratibu wa usimamizi wa dunia inaamuliwa na nchi zote duniani badala ya nchi moja ya Marekani tu. China siku zote inaunga mkono kithabiti mageuzi ya Shirika la biashara duniani WTO, pia inasisitiza kithabiti kuwa mageuzi hayo yanapaswa kulinda thamani kuu ya mfumo wa biashara ya pande nyingi, kulinda maslahi ya maendeleo kwa nchi na sehemu wanachama zinazoendelea na kufuata mfumo wa uamuzi kupitia mazungumzo. China inapenda kutekeleza wajibu unaoendana na uwezo wake wa kiuchumi, na kulinda kithabiti maslahi ya nchi na sehemu wanachama zinazoendelea kwenye shirika la WTO, na China kamwe haikubali hatua yoyote inayoharibu maslahi yake makuu.