Kuvunjika kwa Mkataba wa makombora ya masafa ya kati kutaleta tishio la usalama duniani
2019-08-02 17:25:30| CRI

Muda wa miezi sita wa utaratibu wa kilichodaiwa na Marekani kujitoa kutoka kwenye Mkataba wa Marekani na Russia kuondoa makombora ya masafa mafupi na ya kati (INF) katika nchi hizo mbili umetimia, ikiashiria kuwa, Mkataba huo wenye umuhimu mkubwa katika kulinda usalama wa dunia umevunjika rasmi kuanzia leo tarehe 2 Agosti. Hatua hii ya Marekani ni kitendo chake kingine cha kutekeleza sera za utaratibu wa upande mmoja, hali itakayopunguza kuaminiana kwa usalama wa kimkakati kati ya nchi kubwa duniani, kuongeza ushindani wa kijeshi, na kuleta matishio mapya kwa utaratibu wa usalama wa dunia.

Mkataba huo uliochukuliwa kama ni mkataba wenye ufanisi mkubwa zaidi katika kudhibiti silaha wakati wa vita ya baridi, umeonesha umuhimu mkubwa katika kuhimiza uwiano wa kimkakati kati ya Marekani na Urusi, kupunguza tishio la kukabiliana na vita, na kuzuia kuenea kwa silaha za nyuklia.

Bila shaka kujitoa kwa Markeani katika mkataba huo kutaleta athari kubwa kwa hali ya usalama duniani. Kwanza, kutaharibu zaidi uhusiano kati ya Marekani na Russia, kwani kutokana na kuvunjika kwa mkataba huo, si rahisi kudhania kwamba kama Mkataba mpya kuhusu kupunguza silaha za kimkakati uliopo sasa kati ya Marekani na Russia utaongezwa muda kabla ya mwaka 2021 ambapo mkataba huo utatimiza kazi wake. Pili, Ulaya itakabiliwa na tishio kubwa la usalama. Hivi sasa Marekani imeweka mfumo wa kurusha makombora unaolenga Russia katika nchi za Ulaya Mashariki, Russia haitakuwa na budi kujibu, hali ambayo itasababisha kupamba moto kwa mvutano kati ya Russia na NATO. Tatu, utaratibu wa usalama katika kanda ya Asia na Pasifiki utakuwa na utatanishi mkubwa zaidi. Endapo Marekani itaweka makombora mengi zaidi ya masafa ya kati katika kanda ya Asia na Pasifiki, itasababisha ushindani wa vifaa vya kijeshi kwenye kanda hiyo.

Baada ya Marekani kutangaza kusimamisha kwa upande mmoja Mkataba wa INF, China imekuwa ikitumai Marekani na Russia zitaweza kulinda ufanisi wa mkataba huo kwa kupitia mazungumzo. China siku zote inashikilia sera ya kujilinda, na haipendi kujihusisha na ushindani wa vifaa vya kijeshi. Lakini endapo hali ya nje ya usalama itazidi kuwa mbaya, ni lazima China itachukua hatua zinazohusika ili kulinda maslahi ya usalama ya nchi.

Lakini ukweli wa mambo umethibitisha tena kuwa, kufanya ushirikiano badala ya kuvutana, na kunufaishana badala ya kuonesha umwamba, kutaweza kuhakikisha usalama wa pamoja wa jumuiya ya binadamu.