Shinikizo halitatatua suala lolote
2019-08-02 19:51:29| CRI

Mara baada ya kumalizika kwa duru ya 12 ya mazungumzo ya uchumi na biashara kati ya China na Marekani, Marekani imeinua tena fimbo ya ushuru kutishia kuongeza asilimia 10 ya ushuru dhidi ya bidhaa za China zenye thamani ya dola bilioni 300 za kimarekani zinazouzwa nchini Marekani. Kitendo hicho kimekiuka vibaya makubaliano ya pamoja yaliyofikiwa katika mkutano wa marais wa nchi hizo mbili huko Osaka, Japan,na hakitasaidia kutatua masuala. China inapinga kithabiti na itachukua hatua ya lazima ili kulinda kithabiti maslahi yake.

Ili kukumbusha mchakato wa mazungumzo hayo, kuzungumza wakati wa kushinikiza ni mbinu ya kawaida inayotumiwa na Marekani. Lakini ukweli umethibitisha njia hiyo haisaidii chochote, na sio tu itaharibu fursa ya kuanzisha tena mazungumzo, bali pia haisaidii kutatua masuala na migongano.

Baada ya miezi miwili tangu mazungumzo yakatike, timu za uchumi na biashara za pande mbili zilifanya kwa mara ya kwanza mazungumzo ya ana kwa ana. Kutokana na taarifa zilizotolewa na pande mbili, timu hizo mbili zimekubaliana kuwa zimefanya mawasiliano ya kiujenzi, na kukubali kufanya mazungumzo mengine ya ngazi ya juu mwezi wa Septemba nchini Marekani. Kabla ya hapo, timu hizo mbili zitafanya mazungumzo mengi mwezi wa Agosti kwenye ngazi ya utendaji. Jumuiya kimataifa inazitaka China na Marekani kufuata makubaliano yaliyofikiwa kwenye mkutano wa Osaka na kudumisha mwelekeo wa mazungumzo juu ya msingi wa usawa na kuheshimiana.

Hali ya mwaka mmoja uliopita imethibitisha kuwa hakuna mshindi katika vita vya biashara, kuongeza ushuru hakutatatua ufuatiliaji wa Marekani, bali kunaharibu maslahi za pande mbili za China na Marekani na maslahi ya dunia nzima. Kuinua tena fimbo ya ushuru kwa Marekani sio tu hakulingani na maslahi ya pande mbili, bali pia kunaleta athari na kudhoofisha uchumi wa dunia. Marekani inatakiwa kusahihisha makosa yake kwa wakati, kuhimiza mazungumzo kwa usawa na kuheshimiana, ili kurejesha utatuzi wa masuala katika njia sahihi.