Uchumi wa China una uwezo wa kutosha wa kukabiliana na changamoto
2019-08-14 19:50:53| CRI

Takwimu zilizotolewa leo na Idara Kuu ya Takwimu ya China zinaonesha kuwa, mwezi Julai uchumi wa China umeendelea kukua kwa kasi inayofaa.

Takwimu zilizotolewa na Idara Kuu ya Takwimu ya China zinaonesha kuwa, mwezi Julai thamani ya uzalishaji wa viwanda nchini China imeongezeka kwa asilimia 4.8 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huo. Wakati huohuo, uwekezaji katika sekta za uhifadhi wa mazingira na elimu umeongezeka kwa asilimia 41 na 18.5.

Takwimu hizo pia zinaonesha kuwa sekta ya huduma hususan huduma za kisasa imekua kwa kasi, na katika miezi 7 iliyopita ya mwaka huu, alama ya uzalishaij wa huduma nchini China imeongezeka kwa asilimia 7.1. Kwa upande wa ajira, katika miezi hiyo, China imeongeza ajira milioni 8.67, na kumaliza asilimia 80 ya mpango wa mwaka huu.

Wakati Marekani inaishinikiza zaidi China kutokana na mvutano wa kibiashara, uchumi wa China unakua kwa utulivu, na kuendelea kuwa injini kuu ya uchumi wa dunia. Bila kujali mabadiliko ya mazingira ya nje, China itaendelea kufanya vizuri mambo yake, na kushikilia kukuza mageuzi na kufungua mlango zaidi, ili kutimiza mafanikio ya pamoja na dunia nzima.