Msukumo mpya wahimiza uchumi wa China kupata maendeleo yenye sifa bora
2019-08-15 16:30:14| CRI

Takwimu mpya zilizotolewa na Idara ya Takwimu ya China zimeonesha kuwa, katika miezi saba ya mwanzo mwaka huu, thamani ya nyongeza ya viwanda vya utengenezaji wa teknolojia ya hali ya juu imeongezeka kwa asilimia 8.7 kuliko mmwaka jana wakati kama huu. Pia uwekezaji katika viwanda vya utengenezaji na utoaji wa huduma za teknolojia hiyo umeongezeka kwa asilimia 11.1 na 11.9, hali inayoonesha kuwa msukumo mpya wa uchumi wa China umezidi kuongezeka, imekuwa nguvu muhimu ya kukabiliana na changamoto, na kuhimiza maendeleo ya uchumi yenye sifa bora katika siku za baadaye.

China ikiwa kundi kubwa la pili la kiuchumi duniani, inafanya mabadiliko kutoka "nchi kubwa ya viwanda vya utengenezaji" kuwa "nchi yenye nguvu ya viwanda vya utengenezaji'. Inamaanisha kuwa, China inatafuta kupata ongezeko la uchumi lenye ufanisi mkubwa zaidi, muundo wa kiwango cha juu zaidi na kupata maendeleo endelevu. Kuandaa msukumo mpya na kuzidi kufanya uvumbuzi ni muhimu katika kutimiza maendeleo yenye sifa bora.

Takwimu zimeonesha kuwa, kuanzia mwaka 2015 hadi 2017, wastani wa kigezo cha msukumo mpya wa maendeleo ya uchumi wa China umeongezeka kwa asilimia 28 kwa mwaka, hatua ambayo imeshuhudia ufanisi wa mkakati wa kuhimiza maendeleo kwa njia ya uvumbuzi. Katika miaka ya hivi karibuni, China imeonesha wazi kazi ya utaratibu wa soko, kuchukua hatua mbalimbali za kuhimiza uvumbuzi wa sayansi na teknoljoia, na kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya kuweka msukumo mpya wa ukuaji wa uchumi.

Jambo linalosikitisha watu ni kwamba, baadhi ya nchi za magharibi zimepuuza ukweli kwamba uchumi wa China unafanya mabadiliko huku msukumo mpya ukiimarishwa, na kutoa kauli zisizo na ukweli wowote. Wakati ongezeko la uchumi likipata maendeleo makubwa, wanasambaza "kauli ya tishio la China"; wakati uchumi unapokuwa katika kiwango mwafaka wanaeneza "kauli ya kushuka kwa uchumi wa China", kauli zinazokwenda kinyume cha kanuni ya maendeleo ya uchumi, na pia zinaipaka matope China kwa malengo mabaya.

Ukweli ni kwamba, watu hao wanatakiwa kufuatilia zaidi hali ya uchumi ya nchi zao wenyewe. Gazeti la The Wall Street Journal la Marekani limesema, wanauchumi wanakadiria kuwa katika miezi 12 ijayo, uwezekano wa kushuka kwa uchumi wa Marekani utaongezeka kutoka asilimia 30.1 katika mwezi Julai hadi 33.6, ambacho ni kiwango cha juu zaidi tangu gazeti hilo lilipoanza kufanya uchunguzi huo mwaka 2011.

Hamna mshindi katika vita ya biashara. China inayogeuka kupata maendeleo yenye sifa bora, hakika itachangia msukumo mkubwa zaidi na kutoa fursa nyingi zaidi kwa dunia. Na anayeanzisha vita hiyo atapata hasara kubwa kutokana na vitendo vyake vya utaratibu wa upande mmoja na kujilinda kibiashara.