Hila ya kulifanya suala la kibiashara liwe la kisiasa litashindwa
2019-08-20 16:21:32| CRI

Makamu wa rais wa Marekani Michael Pence jana alihutubia klabu ya uchumi la Detroit akisema, Marekani inawaheshimu sana watu wa China, na haipendi soko la China lipate hasara. Lakini kama nchi hizo zikifikia makubaliano kuhusu suala la uchumi na biashara, China inatakiwa kufuata ahadi zote, ikiwa ni pamoja na kuheshimu ukamilifu wa sheria za Hong Kong kufutia "taarifa ya pamoja ya China na Uingereza" iliyosainiwa mwaka 1984. Hii ni hila ya Marekani ya kulifanya suala la biashara liwe la kisiasa, na kujaribu kuongeza shinikizo kwa China.

Katika zaidi ya mwaka mmoja uliopita, mazungumzo ya kibiashara kati ya China na Marekani yamekwama mara kadhaa kutokana na Marekani kukiuka makubaliano yaliyofikiwa na kutosimamia ahadi zake. Wakati inapoinua fimbo ya ushuru dhidi ya bidhaa za China, inadai kuwa inaheshimu watu wa China, na kutopenda China kupata hasara. Aidha Bw. Pence anapaswa kufahamu vema historia, kwani "taarifa ya pamoja ya China na Uingereza" ilikuwa waraka wa kisiasa wa kupanga mambo ya Hong Kongo katika muda wa mpito ambao ni kati ya mwaka 1984 na 1997. Taarifa hiyo haifai kuwa kisingizio cha Marekani kuingilia mambo ya ndani ya China.

Licha ya suala la Hong Kong, Marekani pia imetangaza kuiuzia Taiwan ndege za kijeshi. Vitendo hivyo vimeonesha kuwa Marekani imeacha sura ya kulinda biashara huria, na kuamua kuchukua mbinu zote kuishinikiza China kuridhia makubaliano yasiyo ya haki ya kibiashara.

Lakini ukweli umethibitisha kuwa, China haitashindwa na shinikizo lolote. Tangu Marekani ianzishe mvutano wa kibiashara zaidi ya mwaka mmoja uliopita, China imedumisha utulivu wa maendeleo ya uchumi, huku uchumi wa Marekani umekuwa na dalili ya kudhoofika. Hivi karibuni hali isiyo ya kawaida ya dhamana ya Marekani imechukuliwa na wawekezaji kama ishara muhimu kwamba uchumi wa Marekani utadidimika.

China siku zote inatetea kutatua suala la biashara kwa mazungumzo, na bila ya kuhusisha masuala mengine, na pia haitarudi nyuma hata kidogo katika masuala makuu. Hila yoyote ya kulifanya suala la kibiashara liwe la kisiasa bila shaka itashindwa.