Uchambuzi: wamarekani kadhaa kukiona cha mtemakuni kwa kauli na vitendo vyao vya kiburi kuhusu Hong Kong
2019-08-21 20:59:17| CRI

Tume ya Masuala ya Sheria iliyo chini ya Kamati Kuu ya Bunge la Umma la China leo imesema baadhi ya wabunge wa Marekani wametoa kauli zisizowajibika na kupotosha ukweli wa mambo na kuunga mkono vitendo vya uhalifu vya watu wenye msimamo mkali mkoani Hong Kong, hatua hii ya kuwachanganya watu mioyoni, inalenga kupinga serikali ya China na kuvugura jamii ya Hong Kong.

Hivi karibuni, spika wa baraza la wawakilishi la bunge la Marekani Nansy Pelosi na seneta Marco Rubio walitoa hoja ya kupitisha "sheria ya haki za binadamu na demokrasia ya Hong Kong" bungeni.

Tangu mwezi Julai, watu wenye msimamo mkali wa Hong Kong wamekuwa wakisababisha migongano ya kimabavu na matukio ya usalama wa umma, kuwashambulia polisi, kuwapiga wanahabari na watalii, kushambulia jengo la bunge la Hong Kong na ofisi ya mawasiliano ya serikali kuu ya China mkoani Hong Kong, kutusi bendera ya taifa, nembo ya taifa na ya mkoa, kuziba barabara, kukaa kwa nguvu uwanja wa ndege…… Vitendo hivyo vimekiuka utawala wa sheria na utaratibu wa Hong Kong, kuharibu vibaya usalama wa umma, kuharibu haki ya msingi ya umma na kukiuka uadilifu na mamlaka ya taifa.

Hata hivyo, Marekani inajificha nyuma kwa kuunga mkono watu hao wenye msimamo mkali, na kwamba sio tu mwanadiplomasia wa Marekani alipatikana akikutana na watu wenye nia ya kuitenganisha Hong Kong na China, bali pia idara za Marekani kutoa msaada wa fedha, kunyoshea vidole ovyo kuhusu suala la Hong Kong na kutishia kuhusisha suala hilo na mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani.

Aliyekuwa mhariri mkuu wa jarida la Wirtschaftswoche la Ujerumani Stefan Baron alitoa makala katika gazeti la Handelsblatt la nchi hiyo kuwa "kama yangetokea Marekani, pengine maandamano hayo yangekuwa yamezimwa mapema."

Kwa muda mrefu, baadhi ya wamarekani wananyoshea vidole ovyo mambo ya ndani ya nchi mbalimbali ikiwemo China, na kauli na vitendo vinajaa upendeleo, ubaguzi, kiburi na hata uchochezi. Lakini Marekani inatakiwa kusikiliza kwa makini alivyosema waziri mkuu wa Singapore Lee Hsien Loong, yaani "Marekani ikiwa nchi yenye nguvu zaidi duniani, inatakiwa kuivumilia China yenye ushawishi mkubwa zaidi na nguvu inayoongezeka. Marekani inatakiwa kukubali kuwa haiwezekani kuzuia kuinuka kwa China, hatua ambayo sio ya busara."

Ndio maana, kama kuna watu wanataka kuharibu ustawi na utulivu wa Hong Kong na hata kukwamisha maendeleo ya China kwa kuzusha machafuko mkoani Hong Kong, watakiona cha mtemakuni.