Marekani kujiumiza kwa kuiuzia silaha Taiwan
2019-08-22 19:44:39| CRI

Wizara ya ulinzi ya Marekani jana iliarifu rasmi bunge kuwa, nchi hiyo inapanga kuiuzia Taiwan ndege 66 za kisasa za kivita aina ya F-16 pamoja na zana nyingine na huduma husika, zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 8. Kitendo hiki kinachokiuka sheria ya kimataifa na kanuni ya kimsingi ya uhusiano wa kimataifa, kuingilia mambo ya ndani ya China, na kukiuka mamlaka na usalama wa China, kinapingwa vikali na China, ambayo itachukua hatua yoyote ya lazima kulinda maslahi yake, ikiwemo kuyawekea vikwazo makampuni ya Marekani yanayoshiriki kwenye mauzo haya ya silaha kwa Taiwan.

Kufuatia kanuni ya "kuwepo kwa China moja duniani" iliyothibitishwa na taarifa tatu ya pamoja ya China na Marekani, Marekani inakubali serikali ya Jamhuri ya Watu wa China ni serikali halali pekee ya China, na Taiwan ni sehemu ya China. Tangu serikali ya Marekani iingie kwenye awamu hii, imekuwa ikiisumbua China mara kadhaa kwa kuiuzia silaha Taiwan.

Madhumuni ya Marekani kufanya hivyo yanajulikana na watu wote. Wakati inapimana nguvu na China katika suala la biashara, huku ikikabiliwa na changamoto ya kisiasa na kiuchumi, Marekani inataka kuishinikiza China kulegeza msimamo wake kwa kutumia suala la Taiwan. Lakini haitashinda kamwe. Kwani China siku zote inatetea kufanya mazungumzo ya kibiashara bila ya kuhusisha masuala mengine, ili kupunguza ugumu wa kufikia makubaliano. Aidha, suala la Taiwan ni maslahi makuu ya China, na haliruhusiwi kuingiliwa na nchi nyingine yoyote.

Kwa upande wa Taiwan, watu wengi wametambua kuwa, badala ya kuleta usalama, kununua silaha kutoka Marekani kutaongeza matishio zaidi kwa Taiwan. Wakati makadirio ya kasi ya ongezeko la uchumi wa Taiwan yamepungua kuwa asilimia 2.08 kwa mwaka huu, gharama ya silaha hizo za Marekani zitaongeza mizigo ya Taiwan, na kudhuru maslahi ya watu wa sehemu hiyo.

Baada ya maendeleo ya kasi ya miaka mingi, China bara imedhibiti kithabiti uhusiano wake na Taiwan, na Taiwan haitaweza kuendelea kuwa kadi ya Marekani ya kuzuia maendeleo ya China. Mustakabali wa Taiwan unategemea China bara, na maisha ya watu wa Taiwan yanategemea ustawi wa taifa la China. Hila ya nchi yoyote ya kusumbua China kupitia suala la Taiwan itajiletea maumivu, na haitakuwa na matokeo mazuri.