China yaendelea kuwa injini ya mafungamano ya kiuchumi duniani
2019-08-27 17:03:18| CRI

China imetangaza orodha mpya kuhusu maeneo ya majaribio ya biashara huria ambayo linahusisha mikoa ya Shandong, Jiangsu, Guangxi, Hebei, Yunnan na Heilongjiang, na hadi sasa idadi ya maeneo ya majaribio ya biashara huria nchini China yamefikia 18. Kwa mara nyingine tena, China imeonesha kwa vitendo halisi kwamba, itasukuma mbele mageuzi na ufunguaji mlango kwa hatua madhubuti, kuelekeza uchumi kupata maendeleo yenye sifa bora, na kuingiza msukumo kwa ajili ya mafungamano ya kiuchumi duniani.

Tangu China ilipoanzisha eneo la majaribio la biashara huria la Shanghai mwaka 2013, miradi 171 ya majaribio ya mageuzi imeanzishwa kote nchini, kampuni zaidi ya laki 6 zimeanzishwa, kati yao elfu 40 zinawekezwa na nchi za nje, na kuvutia asilimia 12 ya mitaji ya kigeni, pia kuchangia asilimia 12 ya thamani ya uagizaji na uuzaji nje wa bidhaa. Faida kubwa zinazoletwa na maeneo ya majaribio ya biashara huria zinaendelea kudhihirika.

Wiki moja iliyopita, Maoni kuhusu kuunga mkono mji wa Shenzhen kujenga eneo la kielelezo la ujamaa wenye umaalumu wa kichina yalitangazwa, na eneo jipya la Lin Gang kwenye eneo la majaribio la biashara huria la Shanghai pia limezinduliwa rasmi. China imetangaza hatua tatu muhimu za ufunguaji mlango ndani ya muda mfupi, hatua ambayo imeonesha imani na nia yake thabiti katika kukuza mageuzi na ufunguaji mlango. Pia imeonesha umuhimu wa kuwa mfano katika kubadili na kupanda ngazi kwa uchumi wake, na kuongeza msukumo mpya katika maendeleo ya uchumi wa China.

Ingawa katika mwaka uliopita, Marekani imechochea na kuzidisha mgogoro wa uchumi na biashara, lakini China imefanya juhudi katika kupanua ufunguaji mlango, na kuendelea kuwa injini yenye nguvu katika kuhimiza mafungamano ya kiuchumi na kujenga uchumi ulio wazi wa dunia. Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, pato la ndani la china liliongezeka kwa asilimia 6.3 na kushika nafasi za mwanzo kati ya makundi muhimu ya kiuchumi. Thamani ya uwekezaji katika viwanda na utoaji wa huduma za teknolojia ya hali ya juu pia iliongezeka kwa asilimia 11.1 na 11.9 katika miezi saba iliyopita. Hali hii imeonesha kuwa, mageuzi na ufunguaji mlango ni njia ya lazima kwa uchumi wa China kubadilika na kupata maendeleo yenye sifa bora.

Maendeleo ya China pia yametoa fursa mpya kwa maendeleo ya dunia. Ripoti kutoka Taasisi ya utafiti ya dunia ya McKinsey imeonesha kuwa, kuanzia mwaka 2000 hadi 2017, kigezo cha utegemezi wa dunia kwa uchumi wa China kimeongezeka kutoka 0.4 hadi 1.2. Tovuti ya habari ya uchumi ya Japan Nihon Keizai Shimbun pia imetoa makala ikisema, nchi na sehemu karibu 200 duniani zimeichukua China kuwa ni mteja muhimu. Hivi sasa, wakati baadhi ya nchi zinafuata utaratibu wa kujilinda kibiashara, China inaonesha msimamo wazi kwa kuchukua hatua thabiti ya kufungua mlango kwamba, inaunga mkono mafungamano ya kiuchumi duniani, na kukaribisha uwekezaji wa nchi za nje ili kunufaishwa kwa pamoja kutokana na fursa za maendeleo za China.