Fimbo ya ushuru ni tishio kubwa kwa ukuaji wa uchumi wa dunia
2019-08-27 19:36:09| CRI

Hivi karibuni baadhi ya watu wa Marekani wamesema hali ya kudai kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za China zenye thamani ya dola bilioni 550 za kimarekani zinazouzwa nchini Marekani, imezidisha hatari ya kupamba moto kwa mikwaruzano ya kibiashara kati ya China na Marekani,na kukosolewa na jumuiya ya kimataifa. Kwenye mkutano wa kilele wa kundi la G7 uliofungwa jana, wenzi wa Marekani pia wameeleza uungaji mkono wa biashara huria. Mwenyekiti wa kamati ya Ulaya Bw. Donald Tusk ameonya kuwa uhusiano wa kibiashara kati ya Marekani na nchi nyingine unaozidi kuwa na wasiwasi, unaweza kuifanya dunia kudidimia.

Historia na hali ya sasa vimethibitisha tena kuwa hakuna mshindi katika vita ya kibiashara, na kuongeza ushuru sio tu hakutatatua migongano, bali pia kunaongeza ugumu wa kutatua masuala. Baadhi ya wamarekani wanaamini matumizi ya nguvu ya fimbo ya ushuru na kuwashinikiza wenzi wa kibiashara ovyo. Matokeo ya hatua hiyo sio tu yanaleta hasara kwa uchumi wa Marekani, bali pia yameathiri imani ya soko la mitaji la kimataifa, mnyororo wa biashara na viwanda na kuwa kikwazo kwa ongezeko la uchumi wa dunia.

Katika mwaka mmoja uliopita, hali ya mikwaruzano ya kibiashara kati ya China na Marekani imekuwa na uhusiano na soko la mitaji. Wakati mazungumzo yakipata maendeleo, soko la hisa la dunia linaongezeka, lakini wakati Marekani ikiinua fimbo ya ushuru, soko hili litashuka mara moja.

Lengo la kuinua fimbo ya ushuru ni kulazimisha kampuni za kigeni zikiwemo za Marekani kuondoka nchini China, ili kukandamiza uchumi wa China. Hatua hiyo imekiuka kwa pande zote kanuni za uchumi wa soko na kanuni za ushindani huria, hali ambayo pia imekata mnyororo wa utoaji na viwanda wa dunia na kuleta hasara kubwa kwa kampuni za kimataifa.

Ushahidi mwingi zaidi umethibitisha kuwa si rahisi kushinda vita ya kibiashara kama baadhi ya wamarekani walivyodhani, kinyume chake ni kwamba vita hiyo imeharibu uchumi wa dunia ukiwemo uchumi wa Marekani.