Makampuni ya Marekani hayataki kuachana na China inayosifiwa kama "Kiwanda cha Dunia"
2019-08-28 20:00:50| CRI

Ili kujibu Marekani kutangaza kuongeza ushuru kwa asilimia 10 dhidi ya bidhaa za China zenye thamani ya dola bilioni 300 za kimarekani zinazouzwa nchini Marekani, hivi karibuni China imechukua hatua za kulipiza kisasi. Baadhi ya wamarekani sio tu wamedai kuzidisha hatua za ushuru, bali pia kuyaamrisha makampuni ya Marekani kuondoka nchini China na kutafuta mpango mbadala. Madai hayo yameshangaza wadau wa sekta ya uchumi wa Marekani, na wameyapinga. Nguvu bora ya kipekee ya China inayosifiwa kama "Kiwanda cha Dunia" haiwezi kuachwa na makampuni ya kimataifa yakiwemo ya Marekani.

China ina watu karibu bilioni 1.4, ambao milioni 400 kati yao ni watu wa kundi lenye mapato ya katikati. Uwezo mkubwa wa soko na matumizi yanayoongezeka siku hadi siku yamelifanya soko la China kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kufanya manunuzi. Shirikisho la wafanyabiashara wa rejareja la Marekani limesema, kuachana na China ikiwa nchi kubwa ya pili kwa uchumi duniani si jambo linaloweza kutimizwa.

Hivyo katika mustakabali ambao uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni FDI kote duniani unapungua, idadi ya wafanyabiashara wanaowekeza nchini China inaendelea kuongezeka. Katika miezi saba ya mwanzo ya mwaka huu, idadi ya makampuni mapya ya kigeni yaliyosajiliwa nchini China imezidi elfu 24, ambayo yametumia fedha za kigeni zaidi ya dola bilioni 74 za kimarekani ikiongezeka kwa asilimia 7.3 ikilinganishwa na mwaka jana.

China ikiwa nchi pekee yenye aina zote za viwanda zilizoorodheshwa na Umoja wa Mataifa, inaweza kutoa mnyororo kamili wa viwanda, utoaji kwa makampuni ya kimataifa, na kuyasaidia kupunguza gharama. Hivi sasa uzalishaji wa aina zaidi ya 200 ya bidhaa za viwandani wa China unachukua nafasi ya kwanza duniani. Mbali na hayo, China pia ina miundombinu bora ikiwemo bandari, barabara kuu na reli na mtandao mzuri wa ugavi wa vitu ambao unaweza kurahisisha makampuni ya kuvuka mipaka kuunganisha viwanda, upande wa utoaji na wateja wa dunia nzima. Hii ni sababu nyingine kwa China kuyavutia makampuni ya kimataifa. Wakati huohuo, China ina nguvukazi ya karibu watu milioni 900, na kila mwaka wanafunzi milioni 8 wanahitimu vyuo vikuu, hivyo idadi ya nguvukazi zenye elimu ya juu nchini China inaongoza katika dunia nzima huku kigezo cha uvumbuzi kikiongezeka hadi kufikia nafasi ya 14 duniani.

Ushahidi umethibitisha kuwa kiwanda cha dunia hakitajengwa ndani ya siku moja. Baadhi ya wamarekani kutaka kukijenga ndani ya muda mfupi, sio tu kunakiuka kanuni za uchumi wa soko na kuvuruga uendeshaji wa makampuni, bali pia hakutaweza kutimizwa. Madai yao yanaweza kuleta vurumai kwenye uchumi wa Marekani na wa dunia.