Kupanda ngazi ya mikwaruzano ya kibiashara kutoweza kutatua masuala
2019-08-30 20:12:37| CRI

Hivi karibuni baadhi ya wamarekani wametangaza tena kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za China zinazouzwa nchini humo na kusababisha kupamba moto kwa hatari ya mikwaruzano ya kibiashara. Hatua hiyo imeenda kinyume na njia sahihi, na kutosaidia kutatua masuala, na haitasaidia maslahi ya China na Marekani wala maslahi ya watu wa dunia nzima.

Katika mwaka mmoja na zaidi uliopita, ili kulinda maslahi halali, imeibidi China kuchukua duru tatu za hatua za kulipiza kisasi. Kutokana na kupanda kwa hatari ya kupamba moto kwa vita vya kibiashara na kuongezeka kwa athari mbaya zinazoletwa na vita hivyo kwa China na Marekani hata dunia nzima, China inaona kuwa kuondoa kuzidi kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za China zenye thamani ya dola bilioni 550 za kimarekani zinazouzwa nchini Marekani na kuzuia kupamba moto kwa vita vya kibiashara, ni kazi ya kwanza.

Takwimu zinaonesha kuwa katika robo ya pili ya mwaka huu kasi ya ongezeko la pato la taifa la Marekani limeshuka hadi kufikia asilimia 2.1 ambayo ni chini kuliko ya robo ya kwanza. Hii inamaanisha kuwa uchumi wa Marekani umepungua katika vita vya kibiashara. Wakati huohuo, hatua ya kuongeza ushuru ya Marekana imewafanya wakulima wa Marekani kupoteza soko kubwa la China. Mbali na hayo, ushuru wa kiwango cha juu unaolenga bidhaa za China pia umehamisishwa kwa wafanyabiashara wa Marekani na wateja, na kuzidi kupandisha gharama za uchumi wa ndani wa Marekani.

Mbali na hayo Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Dunia IMF pia zimetoa maonyo kwa mara nyingi, huku zikisema kama mikwaruzano ya kibiashara ikiendelea kupamba moto, uchumi wa dunia utavutwa katika hali ya kuzorota. Jumuiya ya kimataifa pia imetoa wito Marekani kusimamisha kujilinda kibiashara na kukumbatia utandawazi wa biashara.

Hakuna mshindi katika vita vya kibiashara, China na Marekani zitanufaishana zikishirikiana, na zikipigana kibiashara zitapata hasara. Kutatua migongano kwa njia ya mazungumzo na ushirikiano, sio tu kutazinufaisha China na Marekani, bali pia kutainufaisha dunia nzima.