Hivi karibuni China ilitoa orodha ya mwaka 2019 ya makampuni yake 500 makubwa zaidi. Ikilinganishwa na mwaka jana, makampuni hayo ya mwaka huu yamepata maendeleo ya kasi zaidi, wakati huo huo, yamepanda juu katika mnyororo wa uzalishaji duniani na kuongeza ushawishi wa kimataifa. Kutokana na utatanishi wa hali ya uchumi nchini China na duniani, ni vigumu kwa makampuni ya China kupata mafanikio hayo.
China imetoa orodha ya makampuni yake 500 makubwa zaidi kwa miaka 18 mfululizo, ili kutathmini nguvu ya jumla ya makampuni yake kwa pande zote. Mwaka huu, mapato ya makampuni 500 makubwa zaidi ya China yamezidi dola za kimarekani trilioni 1.12, ambalo ni ongezeko la zaidi ya asilimia 11 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu, wakati huo huo matumizi kwa ajili ya utafiti yamefikia karibu dola za kimarekani bilioni 138, na kuongezeka kwa karibu asilimia 22 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu.
Aidha, makampuni 500 makubwa zaidi ya China ya mwaka huu yameboresha sifa ya maendeleo na kupanda juu katika mnyororo wa uzalishaji duniani. Kwa mfano idadi ya makampuni ya uzalishaji wa hali ya juu na huduma za kisasa imeongezeka kwenye orodha hiyo.
Licha ya hayo, hadhi na ushawishi wa makampuni ya China duniani zimeongezeka kwa mfululizo. Mwaka huu, makampuni 500 makubwa zaidi ya China yameshiriki kwenye ubunifu wa vigezo 1,905 vya kimataifa, na kuongezeka kwa 350 ikilinganishwa na mwaka jana. Kwa mujibu wa orodha ya makampuni 500 makubwa zaidi duniani iliyotolewa Julai, kwa mara ya kwanza idadi ya makampuni ya China kwenye orodha hiyo imekuwa kubwa zaidi kuliko ile ya Marekani.
Hivi sasa kutokana na ongezeko la vitendo vya kujilinda kibiashara na vya upande mmoja, uchumi wa dunia umekabiliwa na changamto kubwa. Sababu kuu ya ukuaji mzuri wa makampuni ya China ni sera ya China ya kukuza mageuzi na kufungua mlango zaidi, pamoja na hatua za serikali za kupunguza ushuru, kuboresha mazingira ya kibiashara, na kuhamasisha makamapuni kufanya uvumbuzi. Mbali na hayo, mafanikio pia yanatokana na juhudi za makampuni hayo yenyewe. Katika muda mrefu uliopita, makampuni ya China yameshikilia njia ya kujiendeleza kwa uvumbuzi, na kuharakisha kujigeuza na kujiboresha.
Makampuni ni sehemu kuu ya uchumi. Ustawi wa makampuni umethibitisha uchumi wa China unaendelea vizuri, na hautashindwa na changamoto yoyote.