Njama ya kuivuruga Hong Kong itashindwa
2019-09-06 19:58:54| CRI

Katika machafuko yaliyotokea hivi karibuni mkoani Hong Kong, baadhi ya waandamanaji wenye msimamo mkali wamedai kuifarakanisha Hong Kong na China, kitendo ambacho kimeonesha wazi sura ya "mapinduzi ya rangi" (Colour Revolution). Nyuma ya njama hiyo, kuna mkono uitwao Mfuko wa Demokrasia wa Taifa wa Marekani NED.

NED ilianzishwa mwaka 1983 na kujidai kuwa ni shirika lisilo la kiserikali, lakini kuanzishwa kwake kuliidhinishwa kisheria na bunge la Marekani, na serikali ya nchi hiyo inagharamia kwa kiasi kikubwa shughuli zake. Kama alivyosema mmoja wa waanzilishi wake Bw. Allen Weninstein, shughuli wanazofanya leo zilifanywa kisiri na Shirika la Ujasusi la Marekani CIA miaka 25 iliyopita.

Tangu mwanzoni mwa karne hii, kutoka Venezuela hadi Ukraine, kutoka Myanmar hadi Syria, NED imekuwa inafanya shughuli mbaya za uchochezi katika nchi na sehemu zaidi ya 100 duniani. Mwaka 2015, idara kuu ya uendeshaji mashtaka ya Russia iliitangaza NED kuwa shirika lisilopendwa kwa sababu shughuli zilizofanywa nayo zilitishia utaratibu wa katiba na usalama wa taifa la Russia.

Vyombo vya habari vya Hong Kong vimesema Taasisi ya Utafiti ya Demokrasia ya Kimataifa ya Marekani iliyo chini ya NED ilianza kutoa pesa kwa makundi ya upinzani mkoani Hong Kong mwaka 1995. Na katika machafuko ya hivi karibuni mkoani Hong Kong, NED imekula njama na watu wa Hong Kong wenye nia ya kuipinga China na kuuvuruga mkoa huo, na kujaribu kufanya "mapinduzi ya rangi, kudhoofisha serikali ya Hong Kong, kupora mamlaka ya usimamizi, kubomoa sera ya nchi moja mifumo miwili na hatimaye wanataka kusambaza "mapinduzi ya rangi" hadi China bara.

Hata hivyo China kamwe hairuhusu shughuli yoyote inayotishia usalama wa mamlaka ya taifa, kuipa changamoto madaraka ya serikali kuu na hadhi ya sheria ya msingi ya mkoa wa utawala maalumu wa Hong Kong, na kuitumia Hong Kong kufanya shughuli mbaya za uharibifu katika China bara.

Hong Kong ni sehemu ya China, na kama machafuko yasiyoweza kuzuiliwa na serikali ya Hong Kong yatatokea, serikali kuu haitakaa kimya, na ina njia nyingi za kutosha na nguvu kubwa ya kutosha kumaliza machafuko.