China yaendelea kuvutia mitaji ya kigeni
2019-09-10 20:05:59| CRI

Maonesho ya biashara na uwekezaji wa kimataifa ya Xiamen mwaka huu yaendelea huko Xiamen, kusini mwa China, na mitaji ya kigeni inayotumiwa katika mikataba iliyosainiwa katika maonesho ya biashara ya mazao ya kilimo ya "Ukanda Mmoja na Njia Moja" imefikia dola bilioni 2.95 za kimarekani. Wakati huohuo, Shirika la Biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa limetoa rasmi "Ripoti ya Uwekezaji wa Dunia 2019" ikionesha kuwa katika mustakabali ambao uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni duniani unapungua kwa miaka mitatu, uwekezaji wa kigeni unaovutiwa na China unaendelea kuongezeka. Hali hii imethibitisha tena kuwa China ni nchi inayovutia uwekezaji mwingi zaidi duniani. Ripoti hiyo imesema, mwaka jana uwekezaji wa moja kwa moja duniani umepungua kwa asilimia 13 ikilinganishwa na mwaka juzi. Lakini uwekezaji wa kigeni unaovutiwa na China umevunja rekodi na kufikia kiwango cha juu zaidi ambao umeongezeka kwa asilimia 4 na kufikia dola bilioni 139 za kimarekani ukiwa unachukua asilimia 11 ya thamani ya jumla ya uwekezaji wa kigeni kote duniani. Ripoti hiyo inakadiria kuwa mwaka huu uwekezaji wa kigeni unaovutiwa na China unatarajiwa kuendelea kudumisha maendeleo ya sifa ya juu zaidi na ya kiwango cha juu zaidi. Takwimu nzuri na makadirio mazuri vimeonesha kuwa mvuto mkubwa wa China kwa uwekezaji wa dunia.

Mvuto huo unatokana na soko kubwa, mnyororo kamili wa viwanda, rasilimali nzuri ya watu, miundombinu na mtandao wa ugavi wenye nguvu nchini China. Mbali na hayo, mvuto huo pia unatokana na nia thabiti ya China kushikilia ufunguaji mlango na kujenga mazingira mazuri kwa mitaji ya kigeni.

Kutokana na mvuto mkubwa, mitaji ya kimataifa inaendelea kupiga kura ya ndiyo kwa China. Miezi saba ya mwanzo ya mwaka huu, mitaji ya kigeni iliyotumiwa nchini China imeongezeka kwa asilimia 7.3. Na Maonesho ya biashara na uwekezaji wa kimataifa ya Xiamen mwaka huu yamevutia makampuni kutoka nchi na sehemu karibu 130 kote duniani, ambayo ni pamoja na makampuni makubwa ya kimataifa.