Uwekezaji katika soko la hisa la A la China wavutia zaidi uwekezaji wa kimataifa
2019-09-23 17:26:14| CRI

Uamuzi wa kipimo cha Dow Jones wa kulihusisha soko la China la ngazi A kwenye kiashiria chake umeanza rasmi leo, hali inayoonesha kuwa, mvuto wa soko la hisa la China na uchumi wa China umekuwa ukiongezeka.

Chanzo kikuu kwa soko la hisa la China kuvutia uwekezaji wa kimataifa ni kwamba, kutokana na nchi zilizoendelea duniani kuchukua sera ya kuongeza utoaji wa fedha, China yenyewe inadumisha sera ya fedha kati ya makundi muhimu ya uchumi duniani, na inatazamiwa kuwa sehemu inayovutia kwa wingi zaidi uwekezaji wa kimataifa kutokana na thamani ya sarafu yake (RMB) kupimwa kwa kiwango cha chini kuliko inavyostahili.

Hivi sasa uchumi wa dunia unakabiliwa na shinikizo la kudorora kutokana na kufufuka kwa utaratibu wa kujilinda kibiashara na vitendo vya upande mmoja. Kutokana na hali hii, mitaji ya kimataifa inazingatia soko la hisa la A kutokana na imani yao juu ya ukuaji wa uchumi wa China. Kama mwanzilishi wa mfuko wa Bridgewater Ray Dalio alivyosema mwezi Agosti kwamba, China, ambayo ni nchi inayofuata sera ya muda mrefu ya kufungua mlango kwa nje, imetoa fursa nzuri kwa uwekezaji wa kigeni.

Wakati huo huo, mitaji ya kimataifa pia itasaidia maendeleo ya soko la hisa la China. Uwekezaji wa kigeni utaongeza utulivu wa soko la hisa la China, na pia kuongeza thamani ya uwekezaji. Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, wawekezaji wa nchi za nje wamechukua hisa ya China yenye thamani ya dola za kimarekani zaidi ya bilioni 50, hali ambayo si kama tu imeleta uhai mkubwa kwa soko la China, pia imeonesha imani ya mitaji ya kimataifa kwa uchumi wa China.

Kutokana na hali isiyotabirika ya uchumi duniani, soko la hisa la China limethibitisha uhai na mustakabali wa uchumi wa China, na kuingiza utulivu kwa masoko ya hisa duniani na uchumi wa dunia. Inawezekana kuwa, kuwekeza mapema nchini China imekuwa mkondo wa kimataifa.