Marekani kuingilia mambo ya ndani ya Hongkong kunaharibu maslahi ya nchi nyingine na kujidhuru yenyewe
2019-09-26 20:35:33| CRI

Kamati ya mambo ya nje ya Baraza la chini na la juu la bunge la Marekani jana ilipitisha Mswada wa haki za binadamu na demokrasia kuhusu Hong kong, kwa kisingizio cha "haki za binadamu" na "demokrasia", na kuunga mkono kwa uwazi watu wenye siasa kali na matumizi ya kimabavu mkoani Hongkong, kuingilia kati kwa nguvu mambo ya ndani ya China, kukiuka vibaya sheria za kimataifa na msingi wa kanuni ya uhusiano wa kimataifa, hatua ambayo imefichua makusudi mabaya ya baadhi ya wamarekani kuivuruga Hongkong na kuzuia maendeleo ya China. China inalaani vikali na kupinga kithabiti hatua hiyo.

Vitendo mbalimbali vya wamarekani hao hakika vitaathiri vibaya maslahi ya nchi nyingine huku ikijidhuru yenyewe, kwani Hongkong ni moja ya wenzi wake muhimu wa kiuchumi na kibiashara barani Asia. Ni lazima Hongkong idumishe ustawi na utulivu, hali hiyo italingana na maslahi ya pande mbalimbali ikiwemo Marekani. Kupitishwa kwa muswada huo kutatoa ishara na kuongeza kujiamini kwa watu wanaotumia mabavu, ambao wataivuruga zaidi Hongkong na kudhuru maslahi yake yenyewe.

Wamarekani hao ni lazima wasimamishe vitendo vya kuhimiza mchakato wa kukagua mswada huo unaohusu Hongkong. Hatua yoyote itakayoidhuru maslahi ya Hongkong na ya China ni lazima ikabiliane na hatua thabiti za kujibu.