Moyo wa mshikamano na kufanya kazi kwa bidii ni chanzo cha "Muujiza wa China"
2019-10-02 16:35:24| CRI

China imefanya maadhimisho makubwa ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China. Kama rais Xi Jinping wa China alivyosema wakati akihutubia katika maadhimisho hayo, mshikamano ni uhakikisho muhimu wa China na wananchi wake kushinda changamoto na kupata mafanikio moja baada ya mengine. Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri yenye kichwa cha "Moyo wa mshikamano na kufanya kazi kwa bidii ni chanzo cha "Muujiza wa China".

Mshikamano ni nguvu. Katika miongo saba iliyopita, wananchi wa China wametafsiri maana halisi ya sentensi hii kwa vitendo. Walivuka vikwazo vilivyowekwa na nchi za magharibi, kushinda maafa makubwa ya kimaumbile, kukabiliana na changamoto katika mchakato wa mageuzi na kufungua mlango, na kufikia mafanikio makubwa. Ikiwa nchi kubwa yenye idadi ya watu karibu bilioni 1.4, China inaweza kuwapatia wananchi wake maisha bora kwa kufanya kazi kwa bidii. Katika miongo saba iliyopita, wachina wamefanikiwa kuifanya nchi yao iwe ya pili kwa nguvu ya kiuchumi duniani, na zaidi ya watu milioni 850 waliondolewa kwenye umaskini uliokithiri.

kuwa na moyo wa mshikamano na kufanya kazi kwa bidii ni mila na desturi za wachina. Katika maelfu ya miaka iliyopita, wachina wameshikamana, kushirikiana, kusaidiana na kusikilizana, na kujenga nchi ya umoja yenye makabila mbalimbali. Moyo wa mshikamano na kufanya kazi kwa bidii pia unatokana na uzalendo wa wachina. Uzalendo umerithiwa na wachina kizazi baada ya kizazi, na umeingia kwenye damu yao. Moyo wa mshikamano na kufanya kazi kwa bidii, pia umeleta imani kwa wachina. Hojaji iliyofanywa hivi karibuni na Shirika la Ipsos Mori la Uingereza inaonesha kuwa, asilimia 22 ya Waingereza, 23 ya Wafaransa na 42 ya Wamarekani wanaona nchi zao zinafuata njia sahihi, ambapo asilimia 94 ya Wachina wanaona hivyo.

China ya hivi leo iko karibu zaidi na lengo kuu la kustawisha taifa kuliko wakati wowote wa zamani, na wakati huohuo, Wachina pia wanafahamu kuwa, China bado ni nchi inayoendelea. Mbali na hayo, China pia inakabiliwa na matishio ya vitendo vya kujilinda kibiashara na vitendo vya upande mmoja, na ongezeko la uwezekano wa kudidimia kwa uchumi wa dunia. Hivyo ni lazima kuimarisha mshikamano wa watu wa makabila na hali mbalimbali na wale walioko nje ya nchi, ili kukabiliana na changamoto za nje, na kupata nguvu mpya ya kuhimiza maendeleo ya China.

Mwishoni mwa mwaka jana, Gazeti la New York Times la Marekani lilitoa makala likisema, huenda hatua ya kusonga mbele ya China iko katika kipindi cha mwanzo tu. Wachina wanaoshikamana na kufanya kazi kwa bidii watafanya miujiza mingi zaidi ya maendeleo, na kuleta fursa nyingi zaidi kwa dunia katika siku za baadaye.