China yatoa onyo kwa kamishina wa NBA kutochanganya "kauli inayoharibu mamlaka ya nchi" na "uhuru wa kutoa maoni"
2019-10-09 17:27:22| CRI

Hivi karibuni mkuu wa Timu ya The Houston Rockets ya Marekani Daryl Morey alitoa kauli ya kuunga mkono waandamanaji katika mkoa wa Hongkong na kukataa kuomba radhi. Naye kamishina wa Ligi ya Mpira wa Kikapu Adam Silver alitangaza hadharani kuunga mkono haki ya Morey ya kutoa maoni yake kwa uhuru. Tarehe 8 Oktoba, chaneli ya michezo ya Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG lilitoa taarifa kwa mara nyingine tena kusimamisha mpango wa kutangaza michezo ya NBA. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China ameeleza bayana kwamba, haistahili kufanya mawasiliano na ushirikiano na China bila ya kuelewa maoni ya watu wa China.

Ni wazi kwamba kauli za watu kama Adam Silver zinakusudia kuchanganya "uhuru wa kutoa maoni" na "kauli ya kuharibu mamlaka ya nchi na utulivu wa Jamii". Bw. Silver alijitetea kwamba siku zote ligi ya NBA inafuata mtizamo wa kuunga mkono usawa, kuheshimiana na uhuru wa kutoa maoni, lakini msingi huo unatakiwa kufuatwa na pande zote. Kauli yenye makosa aliyotoa Morey haikuonyesha heshima kwa mamlaka ya nchi na taifa la China, na msimamo wa Silver wa kulinda watu wanaolenga kuharibu mamlaka ya nchi nyingine na kuumiza hisia za wananchi wa China haikubaliki. Vitendo na kauli zake vimeharibu mtizamo wa ligi ya NBA.

Mbali na hayo Silver ameweka vigezo viwili dhidi ya "uhuru wa kutoa maoni". Katika taarifa mpya aliyoitoa hivi karibuni, alisema, NBA haitasimamia na kudhibiti wachezaji wake kutoa kauli bila ya kujali inafaa au la. Lakini mwaka 2014, mkuu wa Timu ya Clippers ya NBA Sterling alitozwa faini kwa kuhusishwa na rekodi kuhusu ubaguzi wa rangi, na Silver ndiye aliyetoa faini hii. Lakini sasa Silver anamtetea Morey kwa kisingizio cha "uhuru wa kutoa maoni", ambayo inawatia shaka watu kwa tabia yake. Kwa mara nyingine, China inatoa onyo kwa watu kama Silver kwamba, wachina hawatasalimu amri mbele ya masuala yanayohusu mamlaka ya nchi.

Ligi ya NBA ikiwa ligi ya kwanza ya Marekani iliyoingia nchini China, imepata mafanikio makubwa ya kibiashara nchini China katika miaka 30 iliyopita, na kuwa moja kati ya madaraja kati ya mawasiliano ya utamaduni kati ya China na Marekani. Lakini mafanikio kama hayo yatavunjwa kutokana na watu kama Silver ndani ya siku tatu. Je, wakuu wa NBA watawawezesha watu kama hao kuendelee na vitendo vyao?

Watu kama Silver wanatakiwa kujisahihisha mapema, na kuomba radhi kwa moyo wa dhati kwa mashabiki wa China. Lakini ikiwa wanaendelea na vitendo vyao basi watajiadhibu kutokana na makosa yao yenyewe.