Ripoti kuhusu uwezo wa ushindani duniani ya mwaka 2019 iliyotolewa leo kwenye Baraza la Uchumi Duniani huko Geneva, Uswis, imeonesha kuwa, China inashika nafasi 28 kutokana na uwezo wa ushindani.
Ingawa nafasi hiyo ni sawa na ile ya mwaka jana, pointi ya jumla imeongezeka kwa 1.3, hali ambayo imeonesha kuwa China inadumisha uwezo wake mzuri wa ushindani duniani.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, China imepata pointi ya jumla 100 katika upande wa kigezo cha ukubwa wa soko, na kushika nafasi ya kwanza duniani, pia imepata pointi 98.8 katika kigezo cha utulivu wa uchumi wa hali ya jumla. Ripoti hiyo pia imeonesha kuwa, uwezo wa China wa kufanya uvumbuzi umeongezeka kwa kasi na kushika nafasi ya 24 duniani.
Ripoti hiyo vilevile imeonesha umuhimu wa kufungua mlango na kufanya ushirikiano. Kutokana na kuenea kwa utaratibu wa kujilinda kibiashara na vitendo vya upande mmoja, China inaendelea kupanua ufunguaji mlango kwa hatua madhubuti, kutafuta ushirikiano wa kunufaishana, hivyo kulinda uwezo wa ushindani wa uchumi wake duniani, vilevile inachangia katika maendeleo ya uchumi wa dunia.