Ongezeko la hatari ya uchumi wa dunia lahitaji kuimarisha utaratibu wa dunia yenye ncha nyingi
2019-10-10 20:29:17| CRI

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF Bibi Kristalina Georgieva ameonya kuwa, kasi ya kukua kwa uchumi wa dunia ingepungua hadi kiwango cha chini kabisa tangu mwaka 2010 kutokana na athari ya vita vya biashara.

Juu ya hali hiyo ya ongezeko la hatari ya uchumi wa dunia, mawaziri wa fedha wa nchi za Australia, Singapore, Indonesia na Canada wametoa waraka wa pamoja, wakisisitiza kuwa utaratibu wa dunia yenye ncha nyingi ni njia pekee kwa sasa katika kukabiliana na changamoto za kisiasa na kiuchumi duniani.

Tangu rais Donald Trump alipoingia madarakani, serikali ya Marekani imefanya vita ya kibiashara mara kwa mara na kueneza vitendo vya kujilinda kibishara, hali ambayo imeuletea utaratibu wa siasa na uchumi wa dunia changamoto kubwa zaidi. Wakati huohuo, ongezeko la uchumi wa dunia linakabiliana na shinikizo kubwa. Ripoti iliyotolewa mwezi uliopita na Shirika la ushirikiano na maendeleo ya uchumi imesema, makadirio kuhusu ongezeko la uchumi ya mwaka huu yamepunguzwa hadi asilimia 2.9 kutoka asilimia 3.2.

Jumuiya ya kimataifa inapendekeza kutekeleza utaratibu wa dunia yenye ncha nyingi kwa pande zifuatazo:

Kwanza, nchi kubwa zinapaswa kutekeleza wajibu zaidi katika kulinda utaratibu wa dunia yenye ncha nyingi na kanuni za biashara huria.

Pili, nchi kubwa zinapaswa kuendana na maendeleo ya dunia, na kuzifanya nchi zenye uwezo mkubwa wa maendeleo ya uchumi ziwe na haki nyingi zaidi katika kushiriki kwenye utatuzi wa migogoro duniani na kuweka kanuni ya pande nyingi.

Aidha, nchi na makundi mapya husika ya uchumi yanatakiwa kuimarisha imani ya ushirikiano bila kusumbuliwa na wengine, na kuhimiza mafungamano ya kiuchumi, ili kukabiliana na kitendo cha kupinga utandawazi.

Nchi zote duniani zinapaswa kukabiliana na changamoto zinazotukabili, pia zinatakiwa kuwa na imani ya lazima juu ya maendeleo ya siku za usoni. Kama jumuiya ya kimataifa inashikilia utaratibu wa dunia yenye ncha nyingi pamoja na mazungumzo yenye usawa, ufumbuzi mpya utapatikana wa kukinga hatari na kutimiza maendeleo ya kunufaishana.