Kuendeleza biashara za huduma kunahitaji kuimarisha ushirikiano wa kimataifa
2019-10-11 20:45:21| CRI

Shirika la Biashara la Dunia WTO hivi karibuni limetoa ripoti ya biashara ya duania ya mwaka 2019 huko Geneva ikisema, biashara ya huduma imekuwa sehemu yenye uhai mkubwa zaidi inayounda biashara za kimataifa, na kiwango chake kimeongezeka kutoka asilimia 9 ya mwaka 1970 hadi zaidi ya asilimia 20 ya hivi sasa.

Mchango wa biashara ya huduma itaendelea kuongezeka katika miaka zaidi ya kumi ijayo. Kutokana na umuhimu wa biashara hiyo, hali ya kujilinda kibiashara na hatua ya upande mmoja vinavyozidi siku hadi siku, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika sekta ya biashara ya huduma ni muhimu na haraka zaidi.

Maendeleo ya biashara ya huduma yanaweza kuzisaidia nchi mbalimbali kubadilisha mtindo wa maendeleo ya uchumi, kuboresha utaratibu wa viwanda na kuongeza nafasi za ajira. Ripoti hiyo imesema, kiwango cha biashara ya huduma katika pato la taifa kimezidi asilimia 70 kwenye nchi zilizoendelea, na kiwango hicho kimezidi asilimia 50 katika nchi zinazoendelea.

Lakini kutokana na athari zinazoletwa na vitendo vya kujilinda kibiashara na vya upande mmoja, hivi sasa maendeleo ya bishara ya huduma yanapungua na kukosa ushawishi. WTO imesema, nguvu ya kuchochea ongezeko la biashara ya huduma imepungua, hivyo nchi mbalimbali zinatakiwa kufanya juhudi kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, na kutia nguvu mpya kusukuma mbele maendeleo ya biashara hiyo.