China siku zote inalinda usalama wa chakula duniani
2019-10-15 19:21:20| CRI

Serikali ya China jana ilitoa waraka kuhusu usalama wa chakula wa China, ukieleza kwa kina mkakati wa usalama wa chakula wa China, kuonyesha mchango uliotolewa na China katika kulinda usalama wa chakula duniani, na kuhimiza maendeleo ya pamoja, na pia kutoa sera za China katika suala la chakula kwa siku za baadaye.

Katika miaka 70 iliyopita, kutokana na juhudi kubwa, China, ambayo msingi wa kilimo ulikuwa dhaifu na watu wake waliishi maisha magumu, imejitegemea na kufanikiwa kujitosheleza kwa chakula. Mafanikio hayo yanatokana na mkakati wa usalama wa chakula unaotoa kipaumbele kwa soko la ndani la chakula, kuhakikisha uwezo wa uzalishaji, kuagiza chakula kutoka nje kwa kiasi kinachofaa na kutumia teknolojia, ili kufuata njia ya usalama wa chakula yenye umaalum wa kichina. Kujitosheleza kwa chakula kwa China ndio mchango mkubwa zaidi kwa dunia, na mbali na hayo, China inazidi kufungua mlango, kushirikiana na nchi nyingine na kutoa mchango kwa usalama wa chakula duniani.

Wakati dunia inakabiliwa na changamoto ya usalama wa chakula, China imetoa mapendekezo manne ya kuitatua, ambayo ni kuinua uwezo wa uzalishaji, kuimarisha uhifadhi wa chakula ili kujikinga na hali ya dharura, kujenga mfumo wa kisasa wa usambazaji wa chakula na kujitahidi kulinda usalama wa chakula duniani.