Baraza la chini la bunge la Marekani jana lilipitisha "Mswada wa sheria wa mwaka 2019 kuhusu haki za binadamu na demokrasia ya Hong Kong", likiunga mkono watu wenye msimamo mkali na wanaofanya vurugu mkoani Hong Kong, China. Kitendo hicho si kama tu kimekiuka sheria za kimataifa na kuingilia mambo ya ndani ya China, bali pia kitadhuru maslahi ya Marekani.
"Mswada wa sheria wa mwaka 2019 kuhusu haki za binadamu na demokrasia ya Hong Kong" unaitaka serikali ya Marekani kuthibitisha hali ya kujitawala ya mkoa wa Hong Kong kila mwaka, ili kuamua kuendelea kuipa Hong Kong hadhi ya eneo huria ya forodha kufuatia "sheria ya kisiasa ya mwaka 1992 kati ya Marekani na Hong Kong" au la.
Katika miaka 40 iliyopita tangu China na Marekani zianzishe uhusiano wa kibalozi, kuheshimiana mamlaka na ukamilifu wa ardhi, na kutoingiliana mambo ya ndani ni kanuni ya kimsingi ya uhusiano kati ya nchi hizo. Hivi sasa uhusiano kati ya China na Marekani unakabiliwa na utatanishi zaidi kuliko zamani, na pande hizo zinapaswa kutatua maoni tofauti na masuala nyeti kwa njia mwafaka zaidi.
Katika miaka 22 iliyopita tangu Hong Kong kurejeshwa China, "nchi moja na mifumo miwili" imetekelezwa kwa mafanikio makubwa mkoani Hong Kong, na hadhi ya mkoa huo ya kuwa kitovu cha kimataifa cha mambo ya fedha, usafirishaji wa babarini na biashara imeimarika siku hadi siku, na wakazi wa Hong Kong wana haki za demokrasia na uhuru zaidi kuliko wakati wowote uliopita. Hivi sasa watu wengi wametambua kuwa, changamoto inayoikabili Hong Kong si masuala ya haki za binadamu na demokrasia, bali ni kumaliza vurugu na kurejesha utaratibu wa jamii na sheria haraka iwezekanavyo. Badala ya kujali maslahi ya watu wa Hong Kong, madhumuni halisi ya Marekani ni kuzuia maendeleo ya China.
Ikiwa mwenzi muhimu wa kibiashara wa Marekani, kuvuruga Hong Kong hakutaleta manufaa kwa Marekani. Katika miaka mingi iliyopita, urari mzuri wa biashara wa Marekani kutoka Hong Kong ni mkubwa zaidi kuliko wenzi wake wengine wote. Takwimu zinaonesha kuwa, katika miaka 10 iliyopita, urari huo ulifikia dola za kimarekani bilioni 297. Kama Marekani ikipitisha muswada huo, na kuondoa sera nafuu kwa Hong Kong, itajitatiza zaidi katika hali ya kutokuwepo kwa uwiano wa biashara kati yake na nchi za nje.
Licha ya hayo, Marekani ina uwekezaji mkubwa mkoani Hong Kong. Mwaka 2017, thamani ya uwekezaji wa Marekani mkoani humo ilizidi dola za kimarekani bilioni 81. Endapo Hong Kong itakosa utulivu na ustawi, maslahi ya makampuni zaidi ya 1,300 ya Marekani mkoani humo bila shaka yataathiriwa, na wamarekani elfu 85 wanaoishi huko pia wataathiriwa vibaya.
Msukosuko wa Hong Kong hauwezi kuendelea, na sasa ni wakati wa kuumaliza. Kuhusu kitendo cha makosa cha Marekani, China inakiping kithabiti na itachukua hatua za kukijibu. China inaitaka Marekani kutambua vizuri mwelekeo wa historia, na kucha kuingilia mambo ya Hong Kong.