Pendekezo la China lachangia ujenzi wa mustakabali wa pamoja katika mtandao wa Internet
2019-10-21 16:16:31| CRI

Mkutano wa sita wa Mtandao wa Internet duniani umefunguliwa leo mjini Wuzhen, mkoani Zhejiang, China.

Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi ambayo ilichambua kwa kina mustakabali wa maendeleo ya mtandao wa Internet, na kudhihirisha kuwa ni jukumu la pamoja kwa jumuiya ya kimataifa kuendeleza, kutumia na kusimamia vizuri mtandao wa Internet ili kuufanya uhudumie vizuri binadamu. Pia ametoa wito kwa nchi mbalimbali kuhimiza kwa pamoja usimamizi wa mtandao wa Internet duniani, na kujenga Jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya mtandao huo.

Kamishina maalumu wa Idara ya haki miliki za ubunifu ya Umoja wa Ulaya Bw. Guether Marten amesema, China ina mtizamo wa kuangalia siku za baadaye katika usimamizi wa mtandao wa Internet duniani. Ingawa zipo tofauti kati ya nchi za magharibi na China katika masuala husika, lakini zinakabiliwa kwa pamoja na hatari na changamoto katika mtandao wa Internet, na ni mwelekeo kwa jumuiya ya kimataifa kuimarisha ushirikiano katika sekta hiyo.