China na Marekani zahimiza utatuzi wa mvutano wa kibiashara
2019-10-27 18:11:06| CRI

Viongozi wa ujumbe wa China na Marekani katika mazungumzo ya ngazi ya juu kuhusu masuala ya kibiashara wamezungumza kwa njia ya simu, wakikubali kutatua ufuatiliaji wa upande mwingine, na kuthibitisha kumalizika kwa majadiliano ya kiteknolojia kuhusu baadhi ya nyaraka za makubaliano.

Aidha viongozi hao wamekubali kufanya tena mazungumzo kwa njia ya simu hivi karibuni, ili kuharakisha mchakato wa kusainiwa kwa makubaliano ya biashara.

Wachambuzi wanaona baada ya mvutano pamoja na mazungumzo yanayoendelea kwa zaidi ya mwaka mmoja, si rahisi kwa China na Marekani kurejea kwenye njia sahihi ya kutatua suala hilo, na pande hizo mbili zinapaswa kutumia fursa hii, kuzingatia zaidi maslahi ya wazalishaji na wateja, na kufanya jitihada bila kusita kufikia makubaliano ya mwisho.