Maonesho ya kimataifa ya bidhaa zinazoagizwa na China yaonesha mivuto minne ya soko la China
2019-11-09 16:57:38| CRI

Maonesho ya pili ya kimataifa ya bidhaa zinazoagizwa na China yanafanyika mjini Shanghai, China. Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri ya "maonesho ya kimataifa ya bidhaa zinazoagizwa na China yaonesha mivuto minne ya soko la China".

Tahariri hiyo inasema, mvuto wa kwanza wa soko la China ni mahitaji makubwa ya matumizi. Hivi sasa China ni mwezi mkubwa zaidi wa kibiashara wa nchi na sehemu zaidi ya 120 duniani. Takwimu zinaonesha kuwa katika robo tatu zilizopita, thamani ya bidhaa zinazoagizwa na China kutoka nchi mbalimbali duniani ilifikia karibu dola trilioni 1.5 za kimarekani.

Mvuto wa pili wa soko la China ni ubora wa miundombinu. Baada ya maendeleo ya miongo kadhaa, China imejenga miundombinu na mtandao wa uchukuzi wa ngazi ya juu, ambayo inaweza kurahisisha shughuli za wafanyabiashara, na kupunguza gharama zao.

Mvuto wa tatu ni mazingira mazuri ya kibiashara. Ripoti mpya iliyotolewa na Benki ya Dunia imepandisha nafasi ya China kwa 15 duniani katika ubora wa mazingira ya kibiashara.

Mvuto wa mwisho wa soko la China ni uvumbuzi. Kutokana na mchango muhimu unaotokana na teknolojia za kisasa ikiwemo mtandao wa Internet, data kubwa (Big Data) na akili bandia, China yenye rasilimali kubwa ya uvumbuzi inayavutia mashirika mengi ya kimataifa kufanya utafiti wa teknolojia nchini humo.

Tahariri hiyo inasema, katika miaka 15 ijayo, thamani ya bidhaa na huduma zitakazoagizwa na China itazidi dola za kimarekani trilioni tatu na trilioni moja mtawalia. China inayofungua mlango italeta injini kubwa zaidi kwa maendeleo ya uchumi wa dunia.