CIIE yahimiza kufungua mlango na maendeleo kwa pamoja
2019-11-11 17:00:29| CRI

Maonesho ya pili ya Kimataifa ya Uingizaji wa Bidhaa kutoka Nje ya China CIIE yamefungwa mjini Shanghai, China, baada ya kufikiwa kwa makubaliano ya biashara yenye thamani ya dola bilioni 71.13 za kimarekani, ambalo ni ongezeko la asilimia 23 ikilinganishwa na mwaka jana. Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri ya "CIIE yahimiza kufungua mlango na maendeleo ya pamoja".

Tahariri hiyo inasema, Maonesho hayo yameleta injini mpya kwa utandawazi wa uchumi, kuhimiza kufungua mlango, na kutafuta maendeleo kwa pamoja duniani katika pande tatu. Kwanza, maonesho hayo yamehimiza utandawazi wa biashara na ongezeko la uchumi duniani. Ikiwa maonesho ya kipekee ya uingizaji wa bidhaa kutoka nje, maonesho hayo ni hatua kubwa ya China ya kufungua soko lake kwa dunia. Wakati uchumi wa dunia unakabiliwa na ongezeko la vitendo vya upande mmoja na kujilinda kibiashara, maonesho hayo yamehimiza ukuaji wa uchumi wa dunia. Naibu waziri wa mambo ya nje wa Ugiriki Kostas Fragogiannis amepongeza maonesho hayo kwa kuleta fursa kubwa kwa dunia nzima.

Pili, maonesho hayo yamekusanya maoni ya pamoja katika kupinga vitendo vya kujilinda kibiashara na kuunga mkono utandawazi wa uchumi duniani. Ikiwa sehemu ya maonesho hayo, kongamano la kimataifa kuhusu uchumi wa dunia la Hongqiao lililowashirikisha zaidi ya wajumbe 4,000 wa sekta za siasa, biashara na elimu, lilijadili masuala mbalimbali ikiwemo mazingira ya biashara, akili bandia, mageuzi ya Shirika la Biashara Duniani, biashara kupitia mtandao wa internet, na ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja, na kutetea kufungua mlango na kutafuta maendeleo kwa pamoja.

Tatu, maonesho hayo yameonesha mawazo ya "kunufaika kwa pamoja" ya China. Akifungua maonyesho hayo, Rais Xi Jinping wa China, alisisitiza kuhimiza utandawazi wa uchumi duniani kwa kufungua mlango, kushirikisha na kunufaisha pande zote, na kuleta uwiano na mafanikio kwa pamoja. Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Biashara ya Kimataifa cha Umoja wa Mataifa ITC Bw. Arancha Gonzalez amesema, maonesho hayo yameleta fursa nzuri kwa makampuni madogo na yenye ukubwa wa kati ya nchi zinazoendelea kuingia katika soko la China.

Tahariri hiyo inasema, maonesho mawili ya uingizaji wa bidhaa kutoka nje yaliyofanyika nchini China mwaka jana na mwaka huu si kama tu yameonesha soko kubwa na uwezo wa manunulizi wa wateja wa China, bali pia yameonesha nia na hatua halisi ya China ya kufungua mlango, kuunga mkono utandawazi wa uchumi duniani na kulinda biashara huria. Katika siku za baadaye, China itafungua zaidi soko lake, na kutoa fursa nyingi zaidi ya kisoko, ili kutimia maendeleo kwa pamoja.