Ziara ya rais wa China nchini Ugiriki yasaidia kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo
2019-11-12 19:26:41| CRI

Rais Xi Jinping wa China amefanya ziara nchini Ugiriki kuanzia tarehe 10 hadi 12. Katika ziara yake hiyo, viongozi wa nchi hizo mbili wamejadiliana kuhusu jinsi ya kuongeza kuaminiana kisiasa, kuimarisha ushirikiano wa kivitendo, kuhimiza mazungumzo kuhusu ustaarabu, na kufikia maoni muhimu ya pamoja na matunda mengi. Hii imeonesha kuwa majadiliano ya kiustaarabu na ushirikiano wa kunufaishana vinainua ngazi ya uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Ugiriki, jambo litakalowaletea watu wa nchi hizo fursa za maendeleo na kukuza uhusiano kati ya China na Ulaya.

Tangu China na Ugiriki zijenge uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote mwaka 2006, uhusiano wao umeendelea kwa utulivu na kasi. Katika Maonyesho ya Pili ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China yaliyomalizika hivi karibuni, Ugiriki ilishiriki ikiwa mgeni wa heshima, na thamani ya biashara iliyopata ilikuwa ni mara 2.5 kuliko Maonyesho yaliyopita. Ziara hii ya rais wa China nchini Ugiriki baada ya miaka 11 imeelezwa kuwa ni tukio jipya la kihistoria kwa maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Zote zikiwa nchi zenye historia ndefu, sifa ya kipekee ya uhusiano kati ya China na Ugiriki ni kuelewana katika mambo ya ustaarabu. Kwa mfano, rais Xi amesema China na Ugiriki zote zinaunga mkono kuwasiliana na kufunzana katika mambo ya ustaarabu, na zinapinga mgogoro kati ustaarabu tofauti. Amesema pande hizo zinatakiwa kuonesha nguvu bora ya kila upande iliyomo katika kiini cha utamaduni, kutafuta njia ya kuwepo kwa amani kwa staarabu tofauti na watu wa nchi tofauti, na kutoa wazo lenye faida kwa amani ya dunia na maendeleo ya bindamu. Naye Rais Prokopis Pavlopoulos wa Ugiriki amesisitiza kuwa, utamaduni wa jadi wa China na China ya zama za leo ambayo inazidi kufungua mlango wake, kupiga hatua na kupata maendeleo, yote ni ushahidi wa kupinga "kauli ya mgogoro kati ya staarabu tofauti" na "kauli kuwa nchi yenye nguvu lazima inafanya umwamba". Wakati sera ya vitendo vya upande mmoja, kujilinda kibiashara na migongano duniani inapoongezeka, kauli za viongozi wa nchi hizo mbili zenye historia ndefu zina maana kubwa na zimechangia busara na mawazo kuhusu kuondoa tofauti, kuboresha usimamizi wa dunia na kuhimiza maendeleo ya amani.

Katika uhusiano kati ya China na Ugiriki, ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara ni muhimu. Ugiriki ni nchi ya kwanza ya Ulaya iliyoitikia na kuunga mkono pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" la China. Na katika ziara hiyo ya rais Xi, pendekezo la kwanza alilotoa ni kuunganisha pendekezo hilo na mkakati wa Ugiriki wa kujenga kituo muhimu cha usafirishaji bidhaa cha kimataifa, kujenga bandari ya Piraeus kuwa bandari kubwa zaidi ya makontena katika eneo la bahari ya Mediterranean, na kuinua uwezo wa usafirishaji bidhaa katika nchi kavu na baharini kati ya China na Ulaya.

Wakati huohuo, rais Xi amependekeza kupanua wigo wa biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo mbili, kuimarisha mawasiliano ya kitamaduni na kuhimiza uhusiano kati ya China na Ulaya.