Mswada wa Marekani kuhusu suala la Hong Kong ni mchezo wa kisiasa
2019-11-28 19:34:10| CRI

Utawala wa Marekani jana ulisaini "Mswada wa Haki za Binadamu na Demokrasia ya Hong Kong" na kuuidhinisha kuwa sheria. Kitendo hiki cha kuingilia kati mambo ya Hong Kong ambayo ni mambo ya ndani ya China kimepingwa vikali na China na jumuiya ya kimataifa. Shirika kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri yenye kichwa cha "Mswada wa Marekani kuhusu Suala la Hong Kong ni Mchezo wa Kisiasa"

Tahariri hiyo inasema, mswada huo umekiuka sheria za kimataifa na utaratibu wa uhusiano wa kimataifa, na hauna msingi wowote wa kisheria. Marekani imetoa mswada huo kwa kisingizio cha demokrasia na haki za binadamu, ili kuunga mkono watu wanaofanya vurugu, na kitendo hicho kitadhuru jamii na maisha ya watu wa Hong Kong. Pia mswada huo utadhuru maslahi ya Marekani, kwani kwa mujibu wa mswada huo, serikali ya Marekani itatathmini hali ya demokrasia na haki za binadamu mkoani Hong Kong kila mwaka, ili kuamua kama itaipa mkoa huo wa China wadhifa mzuri wa kibiashara, hivyo mswada huo utaathiri biashara kati ya Marekani na Hong Kong. Lakini katika miaka 10 iliyopita, Marekani imepata urari mzuri zaidi kwa biashara kati yake na Hong Kong ikilinganishwa na wenzi wake wengine wa kibiashara.

Tahariri hiyo inasisitiza kuwa, bila kujali hila za Marekani, nia ya China ya kulinda mamlaka, usalama na maendeleo yake haitabadilika.