China yapiga hatua thabiti katika kuelekea kuwa nchi yenye nguvu kubwa kibiashara
2019-12-03 17:17:25| CRI

Hivi karibuni China ilitangaza Mwongozo kuhusu kuhimiza maendeleo yenye sifa bora ya biashara, ikiweka mipango kuhusu kuzidi kuboresha muundo na kuongeza ufanisi na uwezo wa biashara, ili kutimiza maendeleo yenye sifa bora ya biashara na kuielekeza China kuwa nchi yenye nguvu kubwa ya biashara…

Kwanza, muundo wa biashara wa China unatazamiwa kuboreshwa. Hivi sasa bidhaa zinazotegemea idadi kubwa ya wafanyakazi zinachukua sehemu kubwa kati ya bidhaa za aina zote, na thamani mpya ya bidhaa inatakiwa kuongezwa zaidi. Kutokana na hali hii, waraka huo umetangaza kuendeleza biashara ya bidhaa zenye sifa bora, teknolojia ya hali ya juu na bidhaa zenye thamani mpya ya juu, na kuharakisha maendeleo ya akili bandia, hatua ambayo itaongeza uwezo muhimu wa ushindani wa makampuni ya China.

Pili, maendeleo ya biashara ya China yatawekewa msukumo mpya. Kuhimiza maendeleo ya viwanda vipya ni hatua muhimu katika kuongeza injini mpya ya biashara. Waraka huo si kama tu unahimiza makampuni kuanzisha biashara ya kielektroniki katika nchi husika, bali pia inahimiza makampuni makubwa ya biashara ya kielektroniki na usambazaji wa vifurushi kujenga vituo nje ya nchi, ili kuharakisha mchakato wa kuandaa na kuendeleza biashara mpya, na kuongeza ufanisi wa biashara ya jadi.

Aidha, China, ikiwa moja kati ya nchi zinazoendelea duniani, itafanya juhudi kubwa zaidi katika kushiriki kwenye utungaji wa kanuni za kimataifa za biashara. Katika utaratibu wa uchumi na biashara wa dunia ambao uliwekwa na nchi za magharibi, faida kubwa zinazoletwa na mali na faida ndogo ya nguvu kazi zinaleta ukosefu wa haki kwa nchi zinazoendelea. Kwa mujibu wa waraka huo, China italihimiza Shirika la Biashara Duniani (WTO) kufanya mageuzi ya lazima, na kushiriki kwenye mazungumzo ya pande nyingi kuhusu kanuni za biashara.

Mbali na hayo, China inatazamia kujenga utaratibu wenye uwiano zaidi wa biashara. Itazidi kupunguza ushuru wa forodha kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje, na kuandaa maeneo mapya ya kielelezo ya kuhimiza biashara ya uagizaji wa bidhaa.

Kutokana na hayo, utungaji na utekelezaji wa waraka huo utahimiza biashara na uchumi wa China kupata maendeleo yenye sifa bora, na kuongeza utulivu kwa uchumi wa China ambao unakabiliwa na hali zisizotarajiwa.