Kwa nini vyombo vya habari vya magharibi vinakaa kimya kuhusu filamu za kumbukumbu kuhusu Xinjiang
2019-12-08 17:01:13| CRI

Shirika kuu la Utangazaji la China CMG hivi karibuni limetoa filamu mbili za kumbukumbu kuhusu mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea mkoani Xinjiang, China, mashambulizi ambayo yamedhuru vibaya haki za binadamu za watu wa makabila mbalimbali mkoani humo. Filamu hizo zimefuatiliwa sana na watu, ila zimepuuzwa na vyombo vya habari vya nchi za magharibi. CMG imetoa tahariri yenye kichwa cha "Kwa nini vyombo vya habari vya magharibi vinakaa kimya kuhusu filamu za kumbukumbu kuhusu Xinjiang".

Tahariri hiyo inasema filamu hizo zimeonesha video ya baadhi ya mashambulizi ya kigaidi ikiwemo tukio la Julai 5 mwaka 2009 mkoani Xinjiang, shambulizi la kigaidi la Oktoba 28 mwaka 2013 mjini Beijing, na shambulizi la kigaidi la mwaka 2014 dhidi ya abiria katika kituo cha reli mjini Kunming. Vyombo vya habari vya nchi za magharibi vinadai kufuatilia hali ya haki za binadamu mkoani Xinjiang, China, lakini vimekaa kimya kuhusu mashambulizi hayo ya kigaidi yaliyofanywa na magaidi na wafarakanishaji wa Xinjiang.

Wakati Marekani ilitoa "mswada wa mwaka 2019 wa sera ya haki za binadamu mkoani Xinjiang", China imetengeneza filamu hizo mbili za kumbukumbu, ili kufahamisha hali halisi ya Xinjiang. Filamu hizo pia zimewatambulisha watu kuwa, vyombo vya habari vya nchi za magharibi na wanasiasa wa nchi hizo hawajali usalama wa watu wa mkoa wa Xinijang, wanataka kuipaka matope tu serikali ya China kwa visingizio vya haki za binadamu, demokrasia, na uhuru.