Hali ya haki za binadamu nchini Marekani yawekwa wazi katika ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini humo
2019-12-10 20:07:38| CRI

Leo ni Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu. Hali ya haki za binadamu nchini Marekani imewekwa wazi katika ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini humo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Marekani imewashikilia watoto zaidi ya laki moja wa wahamiaji haramu, na kinachoshangaza zaidi, ni kwamba watoto hao wametengwa na wazazi wao. Vyombo vya habari vya Marekani vimesema, tangu mwezi Disemba mwaka jana, watoto wasiopungua watano waliofungwa na Marekani wamefariki.

Hii ni sehemu ndogo tu ya vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu vinavyofanywa na Marekani. Ingawa nchi hiyo inadai kutetea "binadamu wote ni sawa", lakini kwa muda mrefu imekuwa na ubaguzi wa rangi. Katika karne ya 19, jeshi la Marekani lilifukuza na kuwaua Waindio, na kusababisha idadi ya wazawa hao wa asili wa Marekani kuchukua asilimia 2.09 tu ya Wamarekani hivi sasa. Ripoti iliyotolewa mwaka 2017 na Kamati ya Kuondoa Ubaguzi wa Rangi ya Umoja wa Mataifa ilisema, jamii ya Marekani ina hali mbaya ya ubaguzi wa rangi, na inataka wazungu wawe juu zaidi. Hadi mwezi Machi mwaka huu, Umoja wa Mataifa umetoa nyaraka rasmi 22 kuhusu wasiwasi wa hali ya haki za binadamu nchini Marekani, lakini Marekani imezipuuza.

Badala ya kuzingatia hali ya ndani ya haki za binadamu, mara kwa mara Marekani imenyoosha vidole mambo ya nchi nyingine. Hivi karibuni baraza la wawakilishi la bunge la Marekani lilipitisha "Mswada wa mwaka 2019 wa Sera ya Haki za Binadamu za Wauyghur", ili kupaka matope juhudi za China katika kupambana na ugaidi mkoani Xinjiang.

Kuhimiza na kulinda maendeleo ya haki za binadamu ni lengo la pamoja la binadamu. Lakini Marekani inatumia vigeo tofauti na kulifanya suala hilo liwe la kisiasa, kitendo ambacho kinaweza tu kuleta usumbufu kwa masuala ya haki za binadamu duniani.