China ina uwezo wa kuhimiza utekelezaji wa sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili" kupata mafanikio makubwa zaidi
2019-12-20 20:16:12| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba muhimu kwenye hafla ya kusherehekea maadhimisho ya miaka 20 tangu Macau irudi China na kuapisha serikali ya awamu ya 5 ya mkoa wa utawala maalumu wa Macau. Hotuba hiyo imekumbusha mafanikio yaliyopatikana kwenye utekelezaji wa sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili" wa mkoa huo, kueleza mambo manne muhimu juu ya mafaniko hayo, na kutoa matumaini manne kwa maendeleo ya Macau katika siku za baadaye. Wakati huohuo, rais Xi ameweka bayana msimamo thabiti wa kupinga nguvu yoyote ya nje kuingilia kati mambo ya Hong Kong na Macau. Hotuba hiyo imeonesha nia thabiti ya China kuwa na busara na uwezo wa kutekeleza na kuendeleza sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili".

Ukweli umethibitisha kuwa, sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili" sio tu imetatua masuala ya Hong Kong na Macau yaliyosalia kutokana na historia, bali pia imedumisha ustawi na utulivu baada ya mikoa hiyo miwili kurudi China.

Kwenye hotuba yake, rais Xi amekumbusha mafanikio ya utekelezaji wa sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili" kutoka sekta tatu za siasa, uchumi na jamii. Amesema kuwa katika miaka 20 iliyopita, utaratibu wa kikatiba wenye msingi wa katiba na sheria ya msingi ya Macau umekamilika, uchumi wa mkoa huo umetimiza maendeleo makubwa, jamii inadumisha hali ya utulivu na masikilizano na kufungua ukurasa mzuri zaidi wa maendeleo katika historia ya Macau.

Macau ikiwa mkoa wenye eneo dogo, idadi kubwa ya watu na maliasili chache imetimiza maendeleo makubwa ndani ya miaka 20, moja kati ya vyanzo vikuu vyake ni kuelewa na kutekeleza kwa usahihi na kwa pande zote sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili".

Kutokana na juhudi za miaka zaidi ya 30, China imepata uzoefu wa kutosha, kuwa na imani kubwa ya kutosha, kukusanya nguvu zaidi, kuwa na njia nyingi zaidi, busara na uwezo wa kutekeleza na kuendeleza sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili", pia kukamilisha utaratibu wa sera hiyo na kusimamia vizuri zaidi mikoa ya utawala maalumu.