China yapunguza ushuru wa forodha wa bidhaa kutoka nchi za nje
2019-12-23 19:31:20| CRI

Kamati ya kanuni ya ushuru wa forodha ya baraza la serikali la China hivi karibuni imetangaza kupunguza ushuru wa forodha kwa baadhi ya bidhaa zinazoagizwa na China kutoka nchi za nje zikiwemo nyama ya nguruwe, parachichi na vipuri vya magari. Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri yenye kichwa cha "China yapunguza ushuru wa forodha ili kuhimiza ujenzi wa uchumi wa dunia unaofungua mlango"

Tahariri hiyo inasema, kwenye ufunguzi wa maonesho ya pili ya bidhaa zinazoagizwa na China kutoka nchi za nje uliofanyika mwezi Novemba mjini Beijing, rais Xi Jinping wa China alitangaza kuwa, China itaendelea kupunguza ushuru wa forodha na gharama nyingine, ili kuongeza uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nchi za nje. Kupunguza ushuru ni hatua muhimu ya China kutekeleza ahadi yake ya kufungua mlango zaidi na kuleta manufaa ya pamoja kwa dunia nzima kutoka na maendeleo yake. Aidha, China itaendelea kutoa ushuru nafuu kwa nchi zilizo nyuma kimaendeleo zaidi duniani.

Tahariri hiyo inasema inapaswa kuamini kuwa China yenye soko kubwa itatoa jukwaa kubwa zaidi kwa bidhaa bora za nchi mbalimbali duniani, kuwezesha nchi nyingi zaidi haswa zinazoendelea kunufaika maendeleo ya kasi ya uchumi wa China, na kutia nguvu maendeleo ya uchumi wa dunia unaokabiliwa na changamoto kubwa.