Hongkong si kipande cha mchezo wa chesi kwa baadhi ya wanasiasa wa kigeni
2020-01-02 19:14:32| CRI

Hivi karibuni, baadhi ya wanasiasa wa kigeni walimwandikia barua ya pamoja ofisa mwandamizi wa Mkoa wa utawala maalumu wa Hongkong Bibi Carrie Lam, wakilaumu kikosi cha polisi cha Hongkong kinachotekeleza majukumu yake kwa makini ya kulinda utaratibu wa jamii, kushambulia uhuru na utawala wa sheria ambao Hongkong inauonea fahari, na kudai "kuanzisha utaratibu huru wa kimataifa wa uchunguzi", kitu ambacho hakina msingi wowote, na kuingilia kati mambo ya Hongkong kwa uwazi.

Kutokana na hali hii, Januari Mosi mamlaka ya mkoa wa Hongkong ilitoa taarifa ikidhihirisha kuwa barua hiyo ilijaa kauli zinazopotosha ukweli wa mambo, na kwamba baadhi ya watu wa nchi za magharibi wanajaribu kutimiza lengo lao kwa kutumia suala la Hongkong. Ili kuvuruga Hongkong na kuzuia maendeleo ya China, baadhi ya wanasiasa wa kigeni wanatumia njia mbalimbali kuiwekea shinikizo serikali ya mkoa wa Hongkong, na kuingilia kati mambo ya ndani ya China, na barua hiyo ni moja kati ya vitendo hivyo.

Mashitaka yaliyowekwa kwenye barua hiyo yamekwenda kinyume na ukweli wa mambo. Kwa mfano, barua hiyo imesema inafuatilia sana kuongezeka kwa vitendo vya kimabavu vya polisi wakati wa sikukuu ya Krismasi, lakini ukweli ni kwamba, waandamanaji ndio waliorusha mabomu kutoka ghorofani, kufanya uharibifu mkubwa ndani ya maduka, kuwasumbua wakazi, na kuathiri uendeshaji wa kawaida wa maduka. Wanasiasa hao wanapuuza vitendo hivyo, na kulaani askari wa Hongkong wanaotekeleza majukumu kwa kufuata sheria.

Ni wazi kuwa polisi wa Hongkong wamekuwa wakijizuiza, na kufanya juhudi za kurejesha utaratibu wa jamii kutumia kiwango cha chini cha nguvu. Hawakutangulia kuchukua nguvu dhidi ya "waandamanaji", badala yake walijibu vitendo vya ukiukaji wa sheria wa waandamanaji hao kwa nguvu inayostahili, hatua ambayo inalingana na kanuni za kimataifa za haki za binadamu. Tangu mgogoro wa Hongkong ulipotokea, bado hakuna mtu yeyote aliyeuawa kutokana na operesheni ya polisi, badala yake askari polisi 520 wamejeruhiwa wakati wakitekeleza majukumu yao.

Baada ya kupotosha ukweli, wanasiasa hao walitoa dai lisilo na msingi la kuifanya jumuiya ya kimataifa kuanzisha utaratibu huru wa kimataifa wa uchunguzi ili kuchunguza utekelezaji wa sheria wa polisi wa Hongkong, na kutishia kuwawekea vikwazo maofisa wa Hongkong. Wakazi milioni 7.5 wa Hongkong na wananchi bilioni 1.4 wa China kamwe hawatakubali.

Kwenye salamu zake za mwaka mpya, Rais Xi Jinping, aliitakia kila la heri Hongkong na wakazi wa huko, ambayo ni matumaini ya pamoja ya watu bilioni 1.4 ya China. China ina uwezo wa kutosha kulinda vizuri ustawi na utulivu wa mkoa wa utawala wa Hongkong, na wale wanasiasa wa kigeni pia wanapaswa kutambua wazi hali ilivyo, na kusimamisha kuingilia kati kwa matumizi ya nguvu mambo ya Hongkong.