Ongezeko la biashara ya nje ya China kuchangia utulivu wa uchumi duniani
2020-01-14 18:58:27| CRI

Takwimu mpya zilizotolewa na Idara Kuu ya Forodha ya China zimeonesha kuwa, thamani ya jumla ya biashara nje ya China imefikia dola za kimarekani trilioni 4.6 mwaka 2019, ambalo ni ongezeko la asilimia 3.4 kuliko mwaka 2018 wakati kama huo. Kwa kukabiliana na kukwama kwa ongezeko la biashara duniani, hali hii imeonesha uhai wa uchumi wa China, na kutoa mchango muhimu kwa uchumi wa dunia nzima.

Mwaka 2019, kutokana na kuibuka kwa utaratibu wa upande mmoja na kujilinda kibiashara, kiwango cha jumla cha biashara ya nje duniani kilishuka. Takwimu zilizotolewa hivi karibuni kwenye Mkutano wa maendeleo ya biashara wa Umoja wa Mataifa zimeonesha kuwa, biashara ya bidhaa ilipungua kwa asilimia 2.4 mwaka 2019, kiasi ambacho kimeshuka kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 10.7 la mwaka 2017 na ongezeko la asilimia 9.7 la mwaka 2018.

Hata hivyo, mwaka 2019 uagizaji wa bidhaa na mauzo ya bidhaa nje ya China ulipata ongezeko kwa utulivu. Muundo wa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje na kuuzwa nje ya nchi unaendelea kuboreshwa, hatua ya China ya kupanua soko la biashara na nje imepata maendeleo kwa udhahiri, viwanda vya watu binafsi vimeonesha umuhimu mkubwa zaidi, na uwezo wa ushindani wa bidhaa za China zinazouzwa katika nchi za nje pia umeinuka kwa udhahiri.

Mbali na hayo, mwaka 2019 China iliendelea kuchukua hatua za kupunguza ushuru na kuboresha mazingira ya biashara, na kuhimiza ongezeko la biashara nje.

Hivi sasa ukuaji wa uchumi wa dunia unaendelea kupungua, huku hali isiyotabirika ikiongezeka, na mazingira ya nje yanayokabili maendeleo ya biashara nje ya China bado ni magumu. Lakini mwelekeo wa China wa kuboresha muundo wa biashara ya nje, na kuharakisha hatua ya kubadilisha injini ya ukuaji wa uchumi hautabadilika.

Mwaka 2020 umeanza, tunaamini kuwa wakati biashara nje ya China itakapodumisha mwelekeo wa kupata ongezeko kwa utulivu, uwezo wake wa ushindani duniani utazidi kuimarishwa, na pia utatoa mchango muhimu katika ukuaji wa uchumi duniani.