Saa tano usiku jana kwa saa za London, Uingereza ilijitoa rasmi kwenye Umoja wa Ulaya. Tukio hili kubwa la kisiasa baada ya cita baridi linamaanisha nini kwa hali ya siasa nchini Uingereza, uhusiano kati ya Uingereza na Ulaya, na mchakato wa utandawazi barani Ulaya?
Mabadiliko kwa maisha ya watu wa Uingereza
Baada ya kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya, pande hizo mbili zitakuwa na kipindi cha mpito, ambapo mawasiliano ya bidhaa na watu kati yao yataendelea kwa kufuata utaratibu wa kawaida uliopo kwa sasa, hivyo hayatakuwa na mabadiliko makubwa kwa maisha ya watu wa Uingereza.
Katika kipindi hicho, bila ya kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya, Uingereza inatakiwa kufuata kanuni za umoja huo, kutoa mchango wake kwa bajeti ya EU, huku pande hizo mbili zikifanya mazungumzo kuhusu uhusiano wa kibiashara baina yao katika siku za mbele. Jinsi maisha ya Waingereza yatakavyobadilika baada ya kipindi cha mpito itategemea hali ya mazungumzo hayo katika sekta mbalimbali zikiwemo fedha, biashara, uvuvi, uchukuzi wa anga, matibabu na usalama.
Kipindi hicho cha mpito kinatazamiwa kuishia hadi mwishoni mwa mwaka huu wa 2020, na bunge la Uingereza limetunga sheria likipiga marufuku kipindi hicho kurefushwa hadi mwaka ujao wa 2021. Lakini Umoja wa Ulaya una wasiwasi kuwa, ni vigumu kwa pande hizo mbili kufikia makubaliano yanayotosheleza mahitaji ya pande zote ndani ya kipindi hicho.
Athari kwa diplomasia ya Uingereza
Ikiwa ni nchi ya kwanza kuondoka katika Umoja wa Ulaya katika historia, tukio hilo la Uingereza litakuwa ni mtihani mkubwa kwa uhusiano kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya. Ingawa Uingereza imesisitiza kwamba, baada ya kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya, umoja huo bado ni mwenzi wake mkubwa, lakini msukosuko uliojizuka kuhusu kitendo hiki katika miaka kadha iliyopita, umepunguza kwa kiasi uaminifu baina ya pande hizo mbili. Athari zinazowezekana kujitokeza kwa ushirikiano kati yao katika sekta za usalama, bishara na nyinginezo zitategemea matokeo ya mazungumzo kati yao kuhusu uhusiano wao wa kiwenzi katika siku za mbele. Baada ya kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya, Uingereza itahitaji kwa dharura kufufua uchumi, kuinua hadhi yake ya kimataifa, na kutenda kihalisi ujenzi wa utandawazi yake duniani. Hii inamaanisha mbali na kuzungumzia makubaliano ya biashara kati yake na Umoja wa Ulaya, kazi nyingine kubwa itakuwa kusaini upya makubaliano ya biashara huria.
Bw. Martin Wolf, naibu mhariri wa gazeti la Financial Times la Uingereza anaona, sera ya diplomasia ya Uingereza itategemea zaidi nchi nyingine kubwa na Uingereza itapaswa kuchagua itaegemea upande gani katika masuala mengi. Na Bibi Yang Fang, mtaalamu wa China Taasisi ya Uhusiano wa Kimataifa ya China anaeleza kuwa Marekani bado itakuwa mshirika mkuu wa Uingereza, ushirikiano katika usalama na ujasusi ni msingi mkubwa wa uhusiano wa jadi kati ya Uingereza na Marekani, huku mazungumzo kuhusu biashara huria yakiwa nguzo kuu katika maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili katika kipindi kijacho.
Kujiondoa kwa Uingereza kwa EU kutaathiri mshikamano wa Umoja huo?
Baada ya kipindi cha mpito, Uingereza itaondoka katika Jumuiya ya Uchumi ya Ulaya na umoja wa forodha wa Jumuiya ya Ulaya. Wachambuzi wanaona, kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya kunawezekana kuwa mfano wa kuigwa kwa nchi nyingine, na hivyo kuhatarisha mshikamano wa Umoja wa Ulaya na kusababisha kukwama au kupungua nguvu kwa EU.
Kwa upande mwingine, wengine wanaona hii itakuwa ni onyo kwa Umoja wa Ulaya, ambalo umoja huo ungetilia maanani zaidi mageuzi ya ndani, ili kukablinana na matatizo mengi yaliyopo katika mchakato huu wa utandawazi.