"Virusi vya kisiasa" vinavyochafua mfumo wa China lazima viangamizwe
2020-02-06 18:35:33| CRI

Hivi sasa China inatumia kikamilifu ubora wa mfumo wake wa kisiasa, na kufanya juhudi katika kukinga na kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona. Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Bw. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesifu sana mfumo huo wenye nguvu kubwa na ufanisi wake katika mapambano hayo. Lakini waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amekosoa Chama tawala cha China na mfumo wa China ni "tishio la kizama". Wakati China inaposhughulikia hali hii ya dharura, kauli hiyo ya Pompeo, akiwa ofisa mkuu wa kidiplomasia wa nchi yenye nguvu zaidi duniani, si kama tu imekiuka moyo wa ubinadamu, bali pia kuwekea vizuizi ushirikiano kati ya China na Marekani katika kukabiliana na changamoto za pamoja

Bw. Pompeo alisema hayo alipofanya ziara nchini Uingereza hivi karibuni, kutokana na kuwa serikali ya Uingereza ilitangaza kuiruhusu kampuni ya Huawei ya China kushiriki kwenye ujenzi wa mtandao wa 5G nchini humo. Katika miaka kadhaa iliyopita Marekani ilifanya kila iwezalo kukandamiza kampuni za teknolojia ya juu za China kwa kisingizio cha usalama wa taifa, vilevile iliweka shinikizo kwa washirika wake na kuzuia nchi hizo zisifungue soko kwa kampuni za China. Safari hii, Uingereza ilifanya uamuzi huo kwa mujibu wa maslahi yake yenyewe baada ya kufikiria kwa makini faida na hasara, na hili ni pigo kubwa kwa Marekani, hivyo kumfanya atoe malalamiko kwa China.

Ukweli ni kwamba, tangu alipoteuliwa kuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani, kuchafua China kumekuwa mambo ya kawaida kwenye ziara za Bw. Pompeo. Alisambaza nadharia ya "tishio la China", kuingilia kati mambo ya ndani ya China ikiwemo Hong Kong na Xinjiang, kuchafua Chama cha Kikomunisti cha China na Mfumo wa kitaifa wa China. Watu wanaopinga China akiwemo Pompeo wanadhani maendeleo ya China hakika yataharibu faida ya Marekani. Makosa ya kimkakati yatokananyo na msingi wa maoni hayo, yanaendelea kutatiza maendeleo ya uhusiano kati ya China na Marekani. Wanachofanya akina Pompeo ni kutumia ushirikiano wa nchi hizo mbili kufanikisha maslahi yao binafsi ya kisiasa.

Hivi sasa, kwenye mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya korona, China imetumia vizuri manufaa ya mfumo wake. Chini ya maelekezo ya rais Xi Jinping wa China, na uongozi wa tume ya kazi ya kukabiliana na maamubkizi ya Kamati Kuu ya chama tawala CPC, China imechukua hatua za kukinga na kudhibiti kwa pande zote, kuweka mtandao unaofikia mitaani na vijijini, na hii imeonesha ubora wa mfumo wa kijamii wa China. Hatua za China si kama tu zinalenga kulinda usalama na afya za raia wake, bali pia zinalenga kulinda usalama wa afya wa watu wote duniani, na ni hatua zinazowajibika na maslahi ya jumla ya jumuiya ya kimataifa.

Lakini kwa upande wa Marekani, nchi hiyo ilikuwa ya kwanza kuwaondoa wafanyakazi wake wa ubalozi mdogo huko Wuhan, ya kwanza kutangaza kuweka vikwazo dhidi ya Wachina kuingia nchini Marekani, na kuendelea kutengeneza na kueneza hofu duniani. Kauli ya Pompeo yanayochafua mfumo wa China ni sawa na "virusi vya kisiasa", ambavyo vimetatiza ushirikiano wa China na Marekani katika kutatu changamoto zinazoikabili dunia nzima, ndio maana inapaswa virusi hivyo viangamizwe.

Hivi sasa kazi ya kukinga na kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona bado iko katika hali ngumu. Kwa manufaa ya mfumo wake na juhudi za Wachina wote, China ina imani ya kupata ushindi kwenye mapambano hayo. Waswahili husema baada ya dhiki faraja. Tunaamini kwamba baada ya kushinda matatizo kama hayo, China hakika itapata maendeleo mazuri zaidi, na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa kulinda amani na maendeleo ya dunia. Vile vile ubora wa mufmo wa China utatambuliwa na kukubaliwa na watu wengi zaidi.