Tusiache uvumi na ubaguzi kuharibu juhudi za kudhibiti maambukizi ya virusi
2020-02-09 19:53:05| CRI

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Dr. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema shirika lake si kama tu linajitahidi kuzuia uenezi wa virusi vipya vya korona, bali pia linapambana na watu wanaoeneza habari zisizo sahihi na kuharibu juhudi za kukabiliana na virusi kwenye mtandao wa Internet na wale wanaotoa nadharia za njama. Amesisitiza kuwa habari zisizo sahihi zimefanya kazi za madaktari ziwe ngumu zaidi, na kuathiri vibaya ufuatiliaji wa watu wanaotunga sera, na kuchochea vurugu na hofu miongoni mwa watu, hivyo WHO sasa inaunda timu ya kutoa habari sahihi ili kuzuia uenezi wa uvumi.

Hakika kauli hiyo na hatua zitakazochukuliwa na WHO zina maana kubwa kwa kuzuia usambazaji wa uvumi na kusaidia mapambano dhi ya maambukizi ya virusi vipya ya korona.

Baada ya kulipuka kwa virusi hiyo, China imethibitisha virusi hivi ndani ya muda mfupi, kukabidhi utaratibu wa jeni za virusi hivi kwa WHO na nchi nyingine, kutangaza hali ya maambukizi kwa uwazi, na kuchukua hatua mara moja kudhibiti uenezi wa virusi hivi. Hatua za China zimesifiwa na jumuiya ya kimataifa. Lakini baadhi ya wanasiasa na vyombo vya habari vya nchi za Magharibi walitoa habari nyingi feki na nadharia ya njama, kupaka matope sifa ya China, kuongeza hofu ya watu, kudhuru maslahi ya Wachina walioko ng'ambo na watu wenye asili ya Asia, na kuathiri vibaya ushirikiano wa kimataifa katika kupambana na virusi hivi.

Virusi ni adui wa pamoja wa binadamu. China imechukua hatua kali kwa pande zote ili kuwalinda watu wake na watu wote duniani.